Wakimbizi wa Cameroon huko Nigeria taabani
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, limeshtushwa na ongezeko la idadi ya wakimbizi wa Cameroon wanaosaka hifadhi Nigeria ambapo idadi yao sasa imefikia 20,000.
Aikaterini Kitidi ambaye ni msemaji wa UNHCR, mjini Geneva, Uswisi amesema hayo akizungumza na waandishi wa habari akisema kuwa taarifa kutoka kwa washirika wao ni kwamba zaidia ya asilimia 95 ya wasaka hifadhi wanakosa huduma muhimu kama chakula na malazi.
Amesema baadhi ya familia wamebakiza mlo mmoja kwa siku moja kutokana upungufu wa chakula.
(Sauti ya Aikaterini Kitidi)
"Hadi sasa ofisi yetu imekuwa ikifanya kazi ya kutoa huduma kwa wakimbizi hawa chini ya mpango wa dharura wa dola 18 milioni. Hata hivyo, hadi sasa hakuna fedha zilizopokelewa, na kusababisha changamoto kubwa na mapungufu katika utoaji huduma."
Na kuhusu ushirikiano baina ya UNHCR na serikali ya Nigeria Bi Kitidi amesema
(Sauti ya Aikaterini Kitidi)
"Mapema mwezi huu, mamlaka nchini Nigeria ilitenga ardhi kwa UNHCR ambayo inapaswa kuruhusu makazi ya wakimbizi hao ili kuhakikisha usalama wao. UNHCR inaendelea kushirikiana mamlaka husika kususu kuhamishia makazi ya wakimbizi angalau kilomita 50 kutoka mpakani, kulingana na sheria za kibinadamu."