Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujio wangu na ushiriki katika Jukwaa la watu wa asili umekuwa na matokeo chanya mashinani-Kiburo

Carson Kiburo kutoka jamii ya watu wa asili ya Endorois nchini Kenya akihojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili UN.
UN News Picha: Assumpta Massoi
Carson Kiburo kutoka jamii ya watu wa asili ya Endorois nchini Kenya akihojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa ya Kiswahili UN.

Ujio wangu na ushiriki katika Jukwaa la watu wa asili umekuwa na matokeo chanya mashinani-Kiburo

Haki za binadamu

Mkutano wa 21 wa Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa asili, UNPFFII mwaka 2022 umefanyika kwenye makao makuu yake New York. Mkutano huo umewakutanisha watu wengi kutoka pembe zote za dunia. Miongoni mwa waliohudhuria ni Carson Kiburo kijana kutoka jamii ya watu wa asili ya Bondel la ufa kaunti ya Baringo nchini Kenya, amezungumza na Grace Kaneiya wa Idhaa hii.