ceni

CENI yamtangaza Tshisekedi rais mteule DRC, Guterres atoa kauli

Tume ya huru ya taifa ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, CENI imemtangaza Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo kutoka chama cha UDPS, kuwa mshindi wa kiti cha urais kufuatia uchaguzi uliofanyika nchini humo tarehe 30 mwezi uliopita wa Desemba.
 

Hatimaye uchaguzi DRC kufanyika leo isipokuwa katika wilaya 5

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, wapiga kura wanachagua Rais, wabunge na magavana katika uchaguzi mkuu ambao wilaya tano nchini humo hazitapiga kura kutokana na sababu za ukosefu wa usalama na mlipuko wa Ebola.

Kila mmoja ana jukumu la kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani-Guterres

Wakati wananchi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wakihesabu saa kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na majimbo unaotarajiwa kufanyika jumapili hii desemba 30, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika taarifa yake aliyoitoa kupitia msemaji wake hii leo mjini New York Marekani, amewasihi mamlaka nchini DR Congo, viongozi wa kisiasa wa pande zote, tume ya uchaguzi CENI na jumuiya za kijamii kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha kunakuwa na mazingira yasiyo na vurugu kusudi siku ya uchaguzi wapiga kura wote wanaostahili waweze kupiga kura zao kwa amani.

Kuahirishwa kwa uchaguzi DRC kuimarishe mazingira ya upigaji kura- Baraza

Wajumbe wa Baraza laUsalama la Umoja wa Mataifa wamesema wametambua uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, CENI ya kuahirisha hadi tarehe 30 mwezi huu uchaguzi wa rais, wabunge na majimbo ambao ulikuwa ufanyike kesho Jumapili.

Uchaguzi mkuu DRC waahirishwa hadi Desemba 30 :CENI

Tume huru ya Taifa ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, CENI leo Alhamisi imetangaza mjini Kinshasa kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 23 Desemba mwaka huu hadi tarehe 30 Desemba 2018.

Uchaguzi uko palepale licha ya moto kuunguza ofisi za - CENI

Moto mkubwa umeteketeza vifaa vya uchaguzi kwenye ofisi za tume huru ya taifa ya uchaguzi, CENI kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Kinshasa

Sauti -
2'1"

13 Desemba 2018

Jaridani hii leo Siraj Kalyango anaanzia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  ambako moto umeteketeza vifaa vya uchaguzi kwenye mji mkuu Kinshasa, siku chache kabla ya uchaguzi mkuu nchini humo, Tume huru ya Taifa ya  Uchaguzi, CENI yazungumza.

Sauti -
11'40"

Licha ya ofisi za CENI Kinshasa kutiwa moto, uchaguzi uko palepale- CENI

Moto mkubwa umeteketeza vifaa vya uchaguzi kwenye ofisi za tume huru ya taifa ya uchaguzi, CENI kwenye mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Kinshasa. 

Kampeni za uchaguzi zikianza DRC, UN yataka kuwepo kwa kuaminiana na amani

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamesema wanaamini kuwa uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC tarehe 23 mwezi ujao wa Disemba ni fursa ya kihistoria kwa uchaguzi wa kidemokrasia na wa amani kwenye nchi hiyo ya Maziwa Makuu barani Afrika.

Uchaguzi wa disemba ni fursa ya kihistoria kwa DRC-UN

Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamehitimisha ziara yao ya saa 72 nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC na kuahidi kuunga mkono mchakato kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi disemba mwaka huu huku wakisihi uchaguzi huo ufanyike kwa uaminifu na amani.