Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa UN na AU zatekeleza ushirikiano kwa vitendo

Walinda amani UN waliovalia kofia za bluu huingiliana na jamii ya wenyeji katika mazingira ya nje yenye vumbi.

Ni mara ya kwanza kwa UNAMID kuweza kufikia maeneo ya milimani ya Jebel Marra ambako ilikuwa vigumu kufikika na kuendesha doria.

UNAMID/Hamid Abdulsalam Angalau sasa doria za UN zinafika huko Jebel Marra.

Sasa UN na AU zatekeleza ushirikiano kwa vitendo

Amani na Usalama

Umoja wa Mataifa, UN na Muungano wa Afrika, AU wameamua kushirikiana kwa kina ili kusaka suluhu kwenye mizozo na hii imeanza kutekelezwa huko Sudan ambapo ujumbe wa pamoja wa viongozi wa UN na AU uko ziarani nchini humo kutathmini utendaji wa ujumbe wa pamoja wa taasisi hizo huko Darfur, UNAMID.

 Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Selemani Semunyu, mwandishi wa habari wa UNAMID kuweza kufahamu kwa muhtasari yaliyojiri wakati wa ziara hiyo ya Jean-Pierre Lacroix ambaye ni mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani za UN na Smail Chergui, Kamishna wa amani na usalama wa AU.