Skip to main content

Vizuizi visivyo rasmi vyadororesha biashara Afrika Mashariki

Kilimo bora Afrika ni mojawapo ya nchi za kunufaisha wakulima katika soko la pamoja.

Dhamira yakuanzisha soko la pamoja la Afrika ni kutumia masoko ya pamoja yaliyopo kama ngazi ya kufikia soko la bara lote la Afrika.

FAO/Olivier Asselin
Kilimo bora Afrika ni mojawapo ya nchi za kunufaisha wakulima katika soko la pamoja.

Vizuizi visivyo rasmi vyadororesha biashara Afrika Mashariki

Ukuaji wa Kiuchumi

Matumaini yanaelekezwa Kigali Rwanda ambako nchi za Afrika zinatarajiwa kutia saini makubaliano ya eneo la biashara huru na hivyo kupanua wigo wa soko la bidhaa barani humo.

Nchi za Afrika zinatarajiwa kutia saini makubaliano ya kuwa na eneo huru la biashara barani humo. Hii inakuja baada ya majadiliano ya muda mrefu wakati huu ambapo tayari maeneo ya ushirika wa kiuchumi. Baadhi ya watu wana hofu kuwa pengine makubaliano hayo hayatakuwa na mashiko huku wengine wakiwa na matumaini makubwa ya mpango huo kuwa utapanua siyo tu wigo wa soko bali pia kufungua fursa za biashara. Kufahamu zaidi kuhusu shaka, shuku na matumaini  ya makubaliano  hayo yakifahamika pia kama CFTA, Priscilla Lecomte wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya uchumi barani Afrika, ECA ofisi ya kikanda huko Kigali, Rwanda amezungumza na Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania Balozi Augustine Mahiga kando mwa mkutano wa viongozi wa Muungano wa Afrika. Kwanza Balozi Mahiga anajibu swali vipi iwapo nchi nyingi za Afrika hazitotia saini makubaliano hayo.