Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ali Mufuruki asema viwanda ndio suluhu ya AfCFTA

Nchi zetu sisi bado hazijawekeza katika kufundisha wataalamu wa kufanya kazi kwenye viwanda.

Uwekezaji madhubuti katika miundombinu baina ya nchi utasaidia kuboresha biashara na kuinua uwezo wa viwanda barani Afrika. Picha: UM

Ali Mufuruki asema viwanda ndio suluhu ya AfCFTA

Ukuaji wa Kiuchumi

Matumaini ya maendeleo ya kiuchumi barani Afrika yamepigiwa chepuo na hatua ya hivi karibuni  ya kupitishwa kwa azimio la Kigali la Muungano wa Afrika linaloridhia kuanzishwa kwa eneo huru la biashara barani humo.

Viongozi wa Muungano wa Afrika wiki hii wamekunja jamvi la kikao chao kisicho cha kawaida huko Kigali Rwanda kwa hatua muhimu ikiwemo ile ya kukubali kuanzisha eneo huru la biashara kwenye bara hilo. Yaelezwa kuwa eneo hilo huru la biashara litakuwa ni kubwa zaidi kuliko eneo lingile lolote la kiuchumi duniani kwa kujumuisha nchi zaidi ya 50. Kuna matumaini makubwa kufuatia hatua hiyo iliyoanzishwa na tamko la utekelezaji la Lagos zaidi ya miaka 40 iliyopita. Priscilla Lecomte wa tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa, barani Afrika, ECA ofisi ya kikanda huko Kigali, Rwanda alitaka kufahamu mapokea ya makubaliano hayo kwa kiingereza African Continental Free Trade Area au AfCFTA. Priscilla amezungumza Ali Mufuruki ambaye ni Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa kundi la kampuni za Infotech nchini Tanzania. Bwana Mufuruki anaanza kwa kuzungumzia mtazamo wa wafanyabiashara kuhusu makubaliano hayo.