Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 MACHI 2024

14 MACHI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo Jumuiya ya Madola anaelezea kinagaubaga mambo ambayo wanapenda kuona yanatekelezwa ili maudhui ya mwaka huu ya CSW68 ya kuwezesha wanawake kiuchumi na hatimaye kutokomeza umaskini yanafanikiwa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za Haiti, Gaza na dawa za kulevya. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakuletea uchambuzi wa neno “KUPWEMKA”

  1. Baada ya Kenya kutangaza kusitisha mpango wake wa kupeleka askari wa kuleta utulivu nchini Haiti hadi pale hali ya kisiasa itakapotengamaa, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kusaidiana katika kuunda operesheni ya usaidizi kwa watu wa Haiti haraka iwezekanavyo.
  2. Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu dawa za kulevya (CND), imeanza mkutano wake hii leo huko Vienna Austria kukagua maendeleo yaliyopatikana katika kushughulikia tatizo la dawa za kulevya duniani na jinsi ya kuhakikisha utekelezaji wa ahadi za kimataifa. 
  3. Na kukiwa na ripoti za kwamba leo Wapalestina 6 wameuawa kwa kupigwa risasi na wengine 83 wakijeruhiwa wakati wakisubiri malori ya misaada huko Gaza, Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Martin Griffiths kupitia ukurasa wa mtandao wa X ametoa wito wa kulindwa kwa operesheni za misaada ya kibinadamu inayohitajika sana Gaza.
  4. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mkuu wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anachambua maana ya neno  “KUPWEMKA”.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
9'58"