Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania inashikamana na ulimwengu kusongesha ajenda ya mazingira: Waziri Jafo

Tanzania inashikamana na ulimwengu kusongesha ajenda ya mazingira: Waziri Jafo

Pakua

Mkutanowa Umoja wa Mataifa wa Baraza la mazingira duniani UNEA6 leo umekunja jamvi jijini Nairobi Kenya baada ya kukutanisha wadau zaidi ya 7000, kutoka nnyanja mbalimbali kwa lengo la kukabiliana na changamoto kubwa tatu zinazoikabili dunia ambazo ni mabadiliko ya tabianchi, upotevu wa bayoanuai na uchafuzi wa mazingira. Viongozi mbalimbali wanaowakilisha nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wamepata fursa ya kuwasilisha taarifa zao na kushiriki katika mjadiliano. Stella Vuzo afisa habari wa kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS hakuachwa nyuma amekuwa akizungumza na wadau mbalimbali wanaoshiriki mkutano huo wa UNEA6 tangu ulipoanza na leo yuko na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) wa Tanzania Dkt. Selemani Jafo na kwanza amemuuliza anachokibeba kutoka kwenye mkutano huo

Audio Credit
Anold Kayanda/Stella Vuzo
Audio Duration
4'38"
Photo Credit
UN News/Stella Vuzo