Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afghanistan: Watoto 683,000 wanufaika na madarasa ya elimu ya kijamii

Afghanistan: Watoto 683,000 wanufaika na madarasa ya elimu ya kijamii

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linafanya kila juhudi kuhakikisha watoto wanapata mahitaji yao ikiwemo elimu. Huko nchini Afghanistan shirika hilo limehakikisha zaidi ya wanafunzi 683,000 wanapata elimu wangali katika mazingira wanayoishi. 

Mtoto Khadija ni mmoja wa wanufaika wa madarasa ya elimu ya kijamii huko nchini Afghanistan. Kabla ya kuanza kwa programu hii inayofadhiliwa na UNICEF mtoto huyu na wenzake walikuwa hawaendi shule.

Hapo awali, tulikuwa tunagombana na marafiki zangu sababu hatukujua kile kilicho bora. Mimi na marafiki zangu tulikuwa tunacheza sehemu yoyote ile hata kwenye uchafu, sababu hatukujua kuwa ni tatizo. 

Lakini baada ya kuandikishwa na kuanza kushiriki katika madarasa ya elimu ya kijamii, Khadija anasema anafurahia mambo anayojifunza shuleni na kushirikiana na wanafunzi wenzake darasani.

Nina jisikia furaha na fahari. Napenda kujifunza hisabati, Dari, ujuzi wa kijamii na kuandika. Ninapokuja shuleni najifunza vitu vingi sana. 

Asilimia 60 ya wanufaika wa programu hii ya madarasa ya elimu ya kijamii inayotolewa kwa wanafunzi 683,000 nchini Afghanistani ni watoto wa kike. 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
1'43"
Photo Credit
© UNICEF/Mark Naftalin