Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafugaji wa nyuki Karamoja wasema mafunzo ya FAO yamewakomboa wao na familia zao

Wafugaji wa nyuki Karamoja wasema mafunzo ya FAO yamewakomboa wao na familia zao

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limewapiga jeki wafugaji wa nyuki na usindikaji wa mazao ya asali wilayani Nakapiripirit katika jimbo la Karamoja nchini Uganda. Kwa  msaada wa vifaa na mafunzo kutoka kwa shirika hilo maisha ya wakulima wa asali wa eneo hilo na familia zao yamebadilika. 

Wilaya ya Nakapiripirit ina mamia ya wakulima wa asali wengi wakiwa katika vikundi vya kijamii na wengine wafugaji nyuki binafsi. FAO ilitambua thamani ya mazao ya asli kwa watu wa Kramoja na ikaanza kuwapa mafunzo kupitia mradi maalum wa ufugaji wa nyuki, kuanzia utundikaji mizinga, urinaji, usindikaji wa mazao ya asali na hata kuwasidia kutafuta masoko. Miongoni mwa waliokumbatia fursa hiyo ni John Lopetangor ingawa anasema si kazi rahisi, 

“Kuna kazi nyingi katika kuezeka mizinga ya nyuki sio watu wote wanaiweza. Kuna wadudu wanapenda kuingia katika mizinga ya nyuki na wakiingia tu hbasi nyuki wanakimbia. Na cha pili ukiwa na mizinginga ni lazima uitembelee kama vile unatembelea ng’ombe na katika mizinga ambayo haina nyuki lazima uhakikishe unajua tatizo ni nini na ufukishe moto hadi uone nyuki wameingia mzingani, usiache tu ukitegemea nyuki wataingia hapo hutopata asali. Na wakati wa ukame mizinga inapaswa kumwagiliwa maji.”

Licha ya changamoto hizo John anaipenda kazi hii, 

“Hii kazi ni kazi ya maana kwa sababu sasa siuzi ng’ombe , siuzi mbuzi kazi yangu sasa hivi ni kuanzia mwezi wa nne mi nashika pesa mkononi tu hadi mwezi wa tisa, nasomesha sasa watoto wangu vizuri kwa sababu ya asali.”

Na faida hiyo si kwa John peke yake Susan Chepsugul naye ni mfugaji binasi wa nyuki aliingia katika mradi na sasa matunda ameyaona, 

“Nilipouza hiyo asali nilipata fedha kidogo ikanisaidia kuweka akiba nikaenda kuongeza mizinga miwili sasa nikapata mizinga mitatu. Na ninapouza hiyo asali pia inanisaidia kulisha watoto, kulima shamba na kununulia watoto nguo. Wakati nilipolima shamba kwa kutumia hela za asali nilipata gunia moja nikaongeza mzinga mwingine nilionunua.”

Kwa mujibu wa FAO mradi huu sio tu wa kuwainua kiuchumi wanajamii hawa bali pia kuhakikisha wanakuwa na mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
2'28"
Photo Credit
FAO Uganda