Mauaji ya waandishi wa habari hufanyika kwenye nchi zenye amani- UN
- Jukumu la waandishi wahabari kufichua ukweli mashakani
- Wanalengwa hasa kwenye nchi zenye amani kwa kusema ukweli
- Nchi ziweke mifumo ya wanaowashambulia wasikwepe sheria
Mauaji ya waandishi wa habari yalipungua mwaka wa 2021 lakini vitisho vya kutisha bado vibebaki - UNESCO
Waandishi wa habari 55 waliuawa katika mwaka uliopita, 2021, uchunguzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu na Utamaduni, UNESCO umeeleza.
Wanahabari wanapolengwa, jamii kwa ujumla ndiyo inalipia gharama-Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kupitia Ujumbe wake alioutoa hii leo mjini New York Marekani kuhusu siku ya leo ya kimataifa ya kutokomeza ukwepaji wa sheria ya uhalifu dhidi ya wanahabari, amesema katika siku ya mwaka huu, dunia vikiwemo vyombo vya habari, juu ya changamoto nyingine, vimekabiliwa na changamoto mpya kabisa ambayo ni COVID-19.