Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 OKTOBA 2023

04 OKTOBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNCTAD na elimu kwa watoto wote. Makala tunarejelea uchambuzi wa ibara ya 10 ya Tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Mashinani tunakupeleka nchini DRC, kulikoni? 

  1. Kamati ya biashara na maendeleo ya Umoja wa Mataifa UNCTAD, imezindua leo ripoti yake kuu ya Biashara na Maendeleo ya mwaka 2023 ambayo inachunguza kuimarika kwa uchumi wa dunia na kutoa utabiri wa kinachotarajiwa. Ripoti inaeleza hatua za kisera zinazopaswa kuchukuliwa ili kulinda uchumi wa dunia kutokana na matatizo ya kimfumo ya siku zijazo.
  2. Katika kuhakikisha hakuna mtoto yeyote anayeachwa nyuma kupata elimu Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF linatekeleza mradi wa kutoa mafunzo kwa walimu nchini Ghana na tayari wanafunzi 37,000 wamenufaika na mafunzo waliopewa walimu wao. Leah Mushi anatuletea taarifa ya Mwalimu Sam mnufaika wa mafunzo yanayofadhiliwa na UNICEF.
  3. Katika mwendelezo wa uchambuzi wa tamko la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75, leo tunaangazia ibara ya 10 ambayo inasema kwamba “Kila mtu mwenye kesi ana haki ya kusikilizwa kwa haki katika mahakama iliyo wazi kwa umma, yenye kujitegemea, huru na isiyo na upendeleo. Ili kufahamu zaidi kuhusu Ibara hii niliwahi kuzungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika, Mhadhiri Mwandamizi wa sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira nchini Tanzania na alianza kwa kuelezea historia ya ibara hiyo.
  4. Katika mashinani Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kushuhudia jinsi masomo ya kujua kusoma na kuandika inavyoelimisha wananchi kuendesha biashara zao.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
11'42"