Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAR: Walinda amani wa UN kutoka Tanzania na Senegal wafanya mazoezi ya pamoja

CAR: Walinda amani wa UN kutoka Tanzania na Senegal wafanya mazoezi ya pamoja

Pakua

Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha 6 kutoka Tanzania (TANBAT 6) na wenzao kutoka kikosi cha polisi kinachotoka Senegal wote wakihudumu chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamuhuri wa Afrika ya Kati (MINUSCA), kwa wiki nzima wamefanya mazoezi ya pamoja ya ulinzi wa amani na kutuliza ghasia hususani wakati nchi hiyo ikijiandaa na uchaguzi wa ngazi mbalimbali ikiwemo kura ya maoni kuhusu katiba.

Wakiwa wamevalia mavazi maalumu na vifaa vingine vya kujikinga, walinda amani wako katika uwanja wa wazi wanajikumbusha nini kinatakiwa kufanyika pale ambapo watu wenye nia ovu wanapowafanyia vurugu wananchi kwa kuziba barabara na hivyo kukwamisha shughuli za kijamii.  

Kiongozi wa zoezi hilo Kapteni Boniface Issack ambaye ni  Afisa wa mafunzo wa TANBAT 06 anaeleza lengo la zoezi hilo,   

Naye Mkuu wa uangalizi kwa wanajeshi walioko chini ya MINUSCA Kanali Mussa Abdalla anafafanua zaidi akisema, "Zoezi hili linaonesha kunapokuwa na tatizo wakati wa uchaguzi waandamanaji wanapokuja kwa lengo la kuharibu, kuzuia mchakato wa uchaguzi na kama wana nguvu sana, kikosi cha kuchua hatua za haraka cha Tanzania na Senegal wanaitwa kufanya kazi na kuwaondosha waandamanaji kwenye eneo na uchaguzi kufanyika sawasawa.”   

Nikiripoti kutoka Beriberati, Mambere Kadei nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, CAR, mimi ni Kapteni Mwijage Inyoma, TANBAT 6. 

TAGS: TANZABAT 06, Jamhuri ya Afrika ya Kati 

Audio Credit
Kapteni Inyoma
Audio Duration
2'51"
Photo Credit
TANBAT 6/Kapteni Inyoma