Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

21 MACHI 2023

21 MACHI 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina nitasalia hapa hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa katika maandalizi ya mkutano wa maji wa mwaka 2023, unaoanza kesho kumsikia Fr. Benedict Ayodi kutoka shirika la kiamatifa la Wakapuchini wa Fraciscan ambao watakuwa na mjadala maalum kuhusu haki ya maji kwa wote katika mkutano huo. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo zikiwemosiku za UN, UNCTAD na Burundi.  Mashinani tunakuletea ujumbe kuhusu misitu.

  1. Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kupinga ubaguzi wa rangi, Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka kila mtu aazimie kutokomeza ubaguzi huu ambao unaendelea kuathiri kila nchi duniani.
  2. Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya Biashara, UNCTAD imetoa ripoti hii leo inayotaka nchi za Afrika zilizo kusini mwa Sahara zishirikiane kuchagiza matumizi ya nishati ikiwemo rejelezi kama njia ya kuimarisha huduma za afya, elimu na kupunguza umaskini.
  3. Na ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa hii leo imesema ina hofu kubwa juu ya ongezeko la msako dhidi ya watetezi wa haki nchini Burundi kufuatia kuswekwa korokoroni hivi karibuni kwa watetezi watano wa haki za binadamu na kufungwa jele kwa mwandishi wa Habari.
  4. Na katika mashinani tutausikia ujumbe kuhusu uhifadhi wa misitu na faida zake.

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
12'48"