Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

30 DESEMBA 2022

30 DESEMBA 2022

Pakua

Jaridani leo Ijumaa ya tarehe 30 mwezi Desemba mwaka 2022 tunakuletea habari za maombolezo na pia ya uteuzi wa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa UNEP.  Makala tunaelekea nchini Kenya katika makazi ya wakimbizi ya Kalobeyei na mashinani tunaangazia haki za wanawake na wasichana Afghanistan.

  1. Ulimwengu umeendelea kuomboleza kwa masikitiko kifo cha mcheza soka wa Brazil Edson Arantes do Nascimento, almaarufu Pelé. Kwa Umoja wa Mataifa Pelé alikuwa mshambuliaji muhimu katika kufanikisha ushindi wa malengo ya Umoja wa Mataifa. Kwa nyakati tofauti akiteuliwa kuwa Balozi Mwema wa mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa kama elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO na kuhudumia watoto UNICEF.
  2. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres Jumanne wiki hii alimtangaza Elizabeth Maruma Mrema kutoka nchini Tanzania kuwa naibu mkurugenzi mtendaji mpya wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa mazingira UNEP
  3. Makala tunaelekea nchini Kenya katika makazi ya wakimbizi ya Kalobeyei kuangazia mradi unaotumia michezo kulinda vijana hasa wa kike dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia.
  4. Na mashinani tuungane na Ramiz Alakbarov, naibu mwakilishi na mratibu mkazi na wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan akisistiza umuhimu wa haki za wanawake kuheshimiwa. 
Audio Credit
Flora Nducha
Sauti
11'6"