Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 DESEMBA 2022

22 DESEMBA 2022

Pakua

Ni Alhamisi ya tarehe 22 mwezi Desemba mwaka 2022 ambapo leo ni kipindi maalumu kwa ajili ya shukrani kwako msikilizaji wetu na pia kutakiana salamu za Christmas. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini Afghanistan, Sudani Kusini na Myanmar.

  1. Zaidi ya watoto milioni 5 nchini Afghanistan wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 5 wamepatiwa chanjo dhidi ya surua ilhali watoto zaidi ya milioni 6 wenye umri wa kuanzia kuzaliwa hadi miaka 5 wamepatiwa chanjo dhidi ya polio katika kampeni ya kitaifa iliyoanza mwezi uliopita wa Novemba hadi tarehe 12 mwezi huu wa Desemba, katika wilaya 329 za majimbo yote 34 ya Afghanistan.
  2. Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya dharura, Martin Griffiths ametangaza kutoa dola million 14 kutoka mfuko mkuu wa dharura wa Umoja huo, CERF kwa ajili ya kupatia misaada ya kibinadamu wananchi wa Sudan Kusini walioathiriwa na ongezeko la mapigano na mafuriko. 
  3. Na Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya Myanmar Tom Andrews amesema pamoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio kuhusu Myanmar, mara ya kwanza tangu mapinduzi ya kijeshi nchini humo, azimio hilo la kusitisha uhasama na kurejesha utawala wa kidemokrasia halitakuwa na maana lisipotekelezwa kwa vitendo.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
12'41"