Jakaya Kikwete

25 Januari 2019

Jaridani hii leo Arnold Kayanda azungumza na Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye ni mjumbe wa Baraza la Wakimbizi duniani, WRC, ni baada ya kuzindua ripoti yao jijini New York, Marekani.

Sauti -
10'41"

Kunahitajika mabadiliko katika mifumo suala la wakimbizi-Baraza la wakimbizi

Baraza la wakimbizi duniani, WRC limetoa wito kufanyike mabadiliko katika mifumo suala la wakimbizi duniani kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu waliolazimika kukimbia ikiwemo walio wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi.

Kikwete asema "baada ya jando ndiyo nilipata viatu."

Kwa mara ya kwanza nilivaa viatu baada ya kutoka jandoni, ni kauli ya Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyotoa wakati akizungumzia kilichomo kwenye kitabu chake Safary yangu kutoka mwanafunzi aliyekwenda shule peku hadi Urais, kitabu kitakachozinduliwa hivi karibuni. 

Sauti -
1'47"

21 Septemba 2018

Kofi Annan aenziwa Umoja wa  Mataifa, Guterres asema hauwezi kumtenganisha Kofi na Umoja wa Mataifa. Tunabisha hodi Sudan Kusini vijana wazungumzia kuhusu amani ya nchi hiyo. Je wanataka nini?

Sauti -
12'1"

Baada ya jando ndio nilipatiwa viatu- Dkt. Kikwete

Kwa mara ya kwanza nilivaa viatu baada ya kutoka jandoni, ni kauli ya Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete aliyotoa wakati akizungumzia kilichomo kwenye kitabu chake Safari yangu kutoka mwanafunzi aliyekwenda shule peku hadi Urais, kitabu kitakachozinduliwa hivi karibuni.

14 Mei 2018

Jaridani leo Flora Nducha anaangazia...

Sauti -
9'54"

Kutegemea msaada ni mtihani kwa elimu ya nchi za kipato cha chini na cha kati:Kikwete

Hali ya kuwa tegemezi wa misaada inadumaza nchi nyingi kiuchumi na hata kijamii, ikiwemo katika maendeleo ya elimu. Sasa nchi masikini na zenye kipato cha wastani zinachagizwa kuondokana na hali hiyo ili kujikwamua na mzunguko wa umasikini ikiwemo elimu duni na jopo la kimataifa la ufadhili kwa ajili ya elimu limezindua ombi la dola bilioni moja kuzisaidia nchi hizo kuepukana na utegemezi.

Katu hatukubali watoto milioni 250 wawe mbumbumbu

Umoja wa Mataifa leo umepokea ombi lililotiwa saini na vijana milioni 1.5 duniani la kutaka uwekezaji zaidi kwenye elimu.

Sauti -
2'50"

Katu hatukubali watoto milioni 250 wawe mbumbumbu- UN

Elimu yasalia ndoto kwa watoto wengi duniani hususan wa kike, sasa hii leo vijana wenzao wamechukua hatua madhubuti.