Mkurugenzi Mkuu wa IAEA aonesha wasiwasi mkubwa kushambuliwa vituo vya nyuklia vya Iran
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA), Rafael Mariano Grossi, leo ameonya vikali kufuatia mashambulizi ya kijeshi ya Israel dhidi ya maeneo ya nyuklia nchini Iran, akiyataja matukio hayo kuwa “ya kutia wasiwasi mkubwa” na kutoa wito kwa pande zote kujizuia ili kuepusha mzozo zaidi.
Mbegu za mimea zapandwa nje na ndani ya kituo cha anga za juu
Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA limesema mbegu za mazao zilizopelekwa kituo cha anga za juu mwezi Novemba mwaka jana tayari zimepandwa eneo la ndani na nje ya kituo hicho na hivyo zinapata miali kamilifu ya anga za juu pamoja na viwango vya juu zaidi vya joto kwenye eneo hilo.
12 JANUARI 2023
Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Kenya kumulika harakati za elimu ikiwa ni kuelekea siku ya elimu duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka IAEA, msaada wa kibinadamu nchini DRC na matokeo ya mkutano wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa. Mashinani tunakwenda nchini Uganda. Katika kujifunza kiswahili tunapata ufafanuzi wa msemo "FUNGA FUNGANYA"
04 OKTOBA 2021
Katika Jarida la Habari hii leo kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea
-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa antonio Guterres akifungua mkutano wa 15 wa kamati ya Umoja wa Mataifa ya maendfeleo na biashara UNCTAD15 mjini Bridgetown Barbados ametoa wito wa kuhakikisha usawa wa biashara, uwekezaji na na kujikwamua vyema na COVID-19
-Ripoti ya kamati huru ya uchunguzi wa haki za binadamu nchini Libya imesema kuna ushahidi kuwa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoweza kuwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu ulitekelewa nchini humo tangu 2016
Mwongozo mpya kuhusu tiba ya saratani kuokoa Maisha ya mamilioni ya watu:WHO/IAEA
Mwongozo mpya kuhusu tiba ya saratani uliotolewa leo na shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na shirika la kimataifa la nguvu za atomiki (IAEA) kuhusu ununuzi na upatikanaji wa vifaa vya mionzi au radiotherapy unaweza kuboresha fursa za chaguo la matibabu ya saratani yanayookoa maisha fursa ambazo bado ni adimu katika sehemu nyingi ulimwenguni.
Melisa Fleming ndio mkuu mpya wa idara ya mawasiliano ya kimataifa UN
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo amemteua Melissa Fleming raia wa Marekani kuwa ndio mkuu mpya wa idara ya mawasiliano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa au DGC. Bi. Fleming anachukua wadhifa huo wa msaidizi wa Katibu mkuu akimrithi Alison Smale raia wa Uingereza ambaye Katibu Mkuu amemshukuru kwa uwajibikaji wake na huduma kwenye shirika la Umoja wa Mataifa.
IAEA kutoa muongozo wa matumizi ya mionzi kutibu saratani ya wanyama
Matumizi ya mionzi katika tiba ya wanyama yanaongezeka kila siku duniani kote huku Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA likitoa utaratibu kwa madaktari wa mifugo kuhusu namna ya kutumia nguvu za nyuklia kwa usalama.
Amano alijitahidi kuhakikisha nyuklia inatumika kwa usalama:Guterres
Yukiya Amano alifanyakazi bila kuchoka kuhakikisha nishati ya nyuklia inatumika tu kwa sababu salama. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika tarifa yake kufuatia kifo cha mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomiki IAEA.
Yukiya Amano hatunaye tena-IAEA
Shirika la kimataifa la nguvu za atomic IAEA, leo j22 julai 2019 limetangaza kwa masikitoko makubwa kifo cha aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Yukiya Amano.