Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 Julai 2020

15 Julai 2020

Pakua

Hii leo tunamulika janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au coronavirus">COVID-19 kwa muktadha mbalimbali ambapo UNICEF inasema suala la maji kwenye janga hili si la uhai tu bali pia ni lazima. IOM nayo inasema wahamiaji si wasambaza virusi bali wako mstari wa mbele kutoa huduma katikati ya janga hili. Nchini Tanzania shirika la Umoja wa Mataifa la mitaji ya maendeleo, UNCDF limesaidia kuchochea maendeleo kwenye halmashauri ya mji wa Kibaha mkoani Pwani na makala tunamulika ubunifu wa kifaa cha kusaidia mgonjwa wa coronavirus">COVID-19 kupumua wakati akipelekwa hospitali, na hii ni kutoka Kenya. Mashinani tunarejea Tanzania katika kijiji cha Mtavira  mkoani Singida. Mwenyeji wako leo ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora nducha
Audio Duration
11'21"