COVID-19 yazidisha changamoto za chakula Uganda
Njanga la virusi vya corona au COVID-19 limewaacha raia wengi nchini Uganda wakiwa na changamoto ya kipato hali ambayo
imechangia kuongeza changamoto ya uhakika wa chakula. Mwandishi wetu wa Uganda John Kibego mevinjari katika maeneo
mbalimbali kuangazia changamotot za upatikanaji wa achakula na lishe wakati huu ambapo mamilioni ya wanannchi wa kipato
cha chini wanakabiliwa na hatua za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona kwa kutokwenda kazini, kufanya biashara na hata
shughuli zingine zinazoweza kuwaingizia kipato cha kukimu mahitaji ya familia zao. Na sasa kwa mujibu wa serikali ya nchi hiyo
hatua za kutotembea zinatarajiwa kuendelea zaidi ya tarehe tano Mei. Je amebaini yapi? ungana naye katika makala hii
inayoangazia pia juhudi za kukabiliana na changamoto hii na mikakati ya kuhakikisha kwamba watu hawatishiwi na njaa kabla au
baada ya corona kutokomezwa.