Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

6 Aprili 2020

6 Aprili 2020

Pakua

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)

ASSUMPTA:Ni Jumatatu 06 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI

1: Karantini za COVID-19 zashamirisha pia ukatili majumbani, tuchukue hatua- Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka wito wa sitisho la ghasia na mapigano alilitoa hivi karibuni liguse pia ghasia zinazokumba wanawake na wasichana majumbani hususan wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Grace Kaneiya na ripoti kamili.
(Taarifa ya Grace Kaneiya)
Guterres amesema hayo katika tamko lake alilolitoa kwa serikali mbalimbali duniani wakati huu ambapo janga la COVID-19 pamoja na kusababisha machungu ya kiuchumi na kiuchumi, limeripotiwa kuleta machungu ndani ya nyumba sehemu mbalimbali duniani, wanawake wengi wakipiga simu za kusaka usaidizi.
(Sauti ya Antonio Guterres)
“Nilitoa wito kumaliza ghasia kila mahali, sasa. Lakini ghasia si katika uwanja wa vita pekee. Kwa wanawake wengi na wasichana, vitisho vimeshamiri pale ambapo panatakiwa pawe salama zaidi kwao. Majumbani mwao.Na hivyo natoa wito mpya leo hii kwa amani iwepo majumbani na katika nyumba, duniani kote.”

Amesema wito huo unatokana na ukweli kwamba, marufuku ya kusalia majumbanj na karantini pamoja na kuzuia  maambukizi ya COVID-19, yanaweza pia kufanya wanawake wawe kwenye mtego na wapenzi wao makatili.

Ni kwa mantiki hiyo ametoa wito kwa serikali,zifanye huduma za kinga ya ukatili dhidi ya wanawake kuwa sehemu muhimu ya mikakati yao ya kitaifa ya kukabiliana na COVID-19, akimaanisha kwamba,
(Sauti ya Antonio Guterres)
“Ziongeze uwekezaji katika huduma za kusaka usaidizi kwa njia ya mtandao pia kuimarisha mashirika ya kiraia. Mifumo ya mahakama iendelee kushtaki wahalifu wa ukatili majumbani. Pia ziandae mifumo ya kutoa tahadhari kwenye maduka ya dawa na vyakula”
Halikadhalika ametaka serikali zitangaze kuwa makazi ya manusura ni huduma muhimu na ziweke njia salama kwa wanawake kusaka msaada bila ufahamu wa waliowatendea uovu akisema kuwa haki za wanawake na uhuru ni muhimu kujenga jamii thabiti na zenye mnepo.

Amekumbusha kuwa kwa pamoja dunia inapopambana ma COVID-19, inaweza na inapaswa kuzuia ukatili popote, kuanzia majumbani hadi uwanja wa vita.

===================================================

2: WFP yapunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi, Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani (WFP) limekata msaada wake wa chakula na pesa kwa wakimbizi zaidi za milioni 1.2 nchini Uganda kutokana na ukata wa ufadhili wakati huu ambapo dunia imezongwa na changamoto ya kupambana na mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19. Haya hapa maelezo zaidi na mwandishi wetu John Kibego kutoka Uganda.
(Taarifa ya John Kibego.)
Shirka hilo limekata msaada wake wa chakula kwa asilimia 30 na pia kwa wale waliokuwa wakipokea pesa taslimu.
Afisa wa mawasilaino wa shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) cnini Uganda Lydia Wamala ameiambia idhaa hii kwamba hatua hiyo imechukuliwa kutokana na pengo la ufadhili la dola milioni 137 za Kimerekani uliotarajiwa mnamo mwaka huu wa 2020.
Amesema hawajawa na chaguo na kuongeza kuwa kuna hatari ya kupunguza msaada huo zaidi kwa asilimia 15 ikiwa hawatapata ufadhili wa angalao dola milioni 96 za Kimarekani mnamo mwaka huu.
Hata hivyo Wamala amesema ukata huu hautaathiri wakimbizi wapya waliowasili katika kipinidi cha miezi mitatu iliopita na pia WFP itaendelea kujitahidi kutoa chakula sitahili kwa watoto wanaokabiliwa na utapiamlo, wajawazito na wanonyonyesha watoto kulingana na ufadhili uliopo.
WFP inaonya kwamba ukosefu wa mahitaji ya msingi kama chakula kwa wakimbizi unadidimiza matumaini na mustakbali wao ukiwaweza hatarini kwa matatizo mengine mengi zaidi.
Je, wakimbizi wamepokeaje hatua hii?
Nimezungumza na mkimbizi Edson Nzeimaana Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambaye sasa anaishi katikamakaazi ya wakimbizi ya Kyangwali.
(Sauti ya Edson Nzeimaana 1)
Na kutoa wito kwa jamii ya kimataifa.
(Sauti ya Edson Nzeimaana 2)
====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: Punde ni mkala ambapo leo tuko Uganda kumulika changamoto za huduma za afya wakati huu wa COVID-19
====================================================

3: Jumuiya ya michezo yakabiliwa na changamoto kubwa sababu ya COVID-19 :UN
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya michezo kwa maendeleo na amani , Umoja wa Mataifa umesema jumuiya ya kimataifa ya michezo inakabiliwa na changamoto kubwa wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona, COVID-19 kwa watu wengi kushindwa kujumuika katika michezo mbalimbali na pia kufanya mazoezi. Flora Nducha na taarifa zaidi
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa mlipuko wa COVID-19 unasambaa kwa kasi katika nchi mbalimbali na hatua za kujitenga kuepuka mikusanyiko zimekuwa ndio maisha ya kila siku ili kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo.
Hatua hizo zimesababishwa vituo vya michezo, vituo vya kufanyia mazoezi, viwanja vya michezo, mabwawa ya umma ya kuogelea, vituo vya kujifunza muziki na maeneo ya watoto kwenda kucheza kufungwa..
 Na hii inamaanisha kwamba “wengi wetu hatuwezi kushiriki mazoezi ya viungo iwe mmoja mmoja au kwa vikundi vya michezo mbalimbali, au shughuli zozote za mazoezi ya viungo, wala kuangalia mashindano ya michezo moja kwa moja.” 
Umesema Umoja wa Mataifa ukiongeza kwamba na matokeo yake “jumuiya ya kimataifa ya michezo inakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na nchi mbalimbali kote duniani kupambana na COVID-19.”
Hata hivyo katika siku hii Umoja wa Mataifa umesisitiza kwamba hatua zote hizo hazimaanisi kwamba “sasa ndio tuache kufanya mazoezi ya viungo kabisa au tuache mawasiliano na makocha, wachezaji wenzetu, wakufunzi na mashabiki wenzetu wa michezo ambao sio tu kwamba wanatusaidia kuhakikisha tuko vyema kiviungo bali pia kijamii.”
Shirika la afya la umoja wa Mataifa WHO linapendekeza dakika 150 ya mazoezi ya wastani au dakika 75 za mazoezi makali kwa wiki au kufanya vyote. 
WHO imesema kuna njia mbalimbali za kuhakikisha watu wanajishuhulisha kiviungo wakati huu wa COVID-19 ikiwemo kutumia nyenzo za bure mtandaaoni na hivyo inawachagiza watu wa rika zote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya aina moja au nyingine wakati huu mamilioni ya watu wakisalia majumbani.
Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa michezo ina uwezo wa kubadili dunia, ni haki ya msingi, nyenzo muhimu ya kuimarisha mshikamano wa kijamii na kuchagiza malengo ya maendeleo endelevu, amani, mshikamano na kuheshimiana.
Siku ya kimataifa ya michezo kwa ajili ya maendeleo na amani huadhimishwa kila mwaka Aprili 6.

 

 
===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA: Sasa ni makala na ambapo tunaungana na mwandishi wetu John Kibego nchini Uganda kuangazia changamoto katika kufikia huduma za afya ambazo zimeibuka kutokana na maagizo mapya yanayolenga kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona au COVID-19 nchini humo.
=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
====================================================

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:

Shukran sana John Kibego kwa makala hiyo.
====================================================
Na sasa ni  mashinani ambapo Mkuu wa Operesheni na vifaa wa WHO, Jan Erik Carsen anafafanua wanavyohaha kuhakikisha shirika la afya la Umoja wa Mataifa, linapeleka vifaa vya kutosha kwa watendaji wake walio mstari wa mbele kukabiliana na janga la virusi vya corona.
 ===================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA:

Shukrani sana Erik Carsen na twawatakia kila la kheri.
==================================================
STUDIO: Play Bridge

ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Tupatane kesho kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York.

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'28"