Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

1 Aprili 2020

1 Aprili 2020

Pakua

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)      

ASSUMPTA:Ni Jumatano 01 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI 

1: Kenya yachukua hatua zaidi kudhibiti COVID-19, wakati wagonjwa wawili wakipona na wapya kuzuka

Wagojwa wawili ambao wamethibitishwa kupona virusi vya corona nchini Kenya wameonekaa hadharani kwa mara ya kwanza leo wakati wakizungumza kwa njia ya video na Rais Uhuru Kenyatta na kuonyeshwa kwenye runinga kadhaa nchini Kenya. Hata hivyo wizara ya afya nchini Kenya imatangaza uwepo kwa wagonjwa 22 zaidi wa virusi vya corana hii leo na kufanya idadi jumla kufikia wagonjwa 81. Jason Nyakundi anayo taarifa kamili

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

Hii ndiyo mara ya kwanza waathiriwa hao wa virusi vya corona kwa majina Brenda na Brian na ambao sasa wamepona wameonekana hadharani.
Brian na Brenda walifanya mazungumzo na rais Kenyatta ambapo Rais aliwashauri wakenya kusaidia katika kuzuia maambukizi ya virusi hivyo hatari.
Brenda ndiye mgonjwa kwanza na Brian mgonjwa wa tatu kupona kutokana na virusi vya Corona nchini Kenya.
Akitangaza hilo waziri wa afya Mutahi Kagwe amewataka wakenya kufuata kanuni zinaohitajika ili kusaidia kupigana na virusi hivyo hatari vya corona.
(SAUTI YA KAGWE 1)
 
Awali waziri Kagwe pia alisema kuwa maambukizi mapya yanatokana na usafiri wa bodaboda, ambao upo katika kila kona ya nchi, ambapo alitoa kanuni mpya kwa waendeshaji wa bodaboda ili kuzuia maambukizi kati yao na wateja wao.
 
Alisema kuwa kwa watakaokaidi kanuni hiyo watalazimishwa na maafisa wa polisi.
 
(SAUTI YA KAGWE 2)
 
 Hadi leo Jumatano wagonjwa waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona nchini Kenya wamefikia watu 81 kwa mujibu wa wizara ya afya baada ya wagonjwa 22 kuthibitishwa leo.
 
Wizara ya afya inasema kuwa wagonjwa 21 kati 22 waliogunduliwa kuwa na virusi vya corona tayari walikuwa katika karantini.
 
Katika upande mwingine wizara hiyo ya afya imeonya kuwa huenda maambukizi yakawa makubwa zaidi kuanzia wiki ya kwanza ya mwezi Aprili.
 
Mkurugenzi katika wizara ya afya Dr Patrick Amoth amesema huenda hata hadi watu 10,000 wakaambukizwa virusi vya Corona nchini Kenya ifikapo mwisho mwa mwezi Aprili.
 
(SAUTI YA AMOTH)

===================================================

2: MONUSCO na harakati za kudhibiti kuenea kwa COVID-19 nchini DRC
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako idadi ya wagonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ambao wamethibitishwa hadi leo hii ni 109 huku 8 (wanane) kati yao tayari wamefariki dunia, Umoja wa Mataifa umechukua hatua kuunga mkono hatua za serikali za kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi hivyo miongoni mwa wananchi wanaowahudumia na wafanyakazi wake.
 
Mathalani ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO umechukua tahadhari hizo na baadhi ya hatua ni  kupunguza doria, kufuta safari zisizo za lazima ndani ya nchi, kufanya mikutano muhimu kwa kutumia teknolojia ya video ili kupunguza hatari zaidi. 
 
Aidha timu ya matabibu kutoka MONUSCO imejiandaa na inafuatilia hali kwa karibu huku wakielezea kile wanachofanya kama anavyofafanua Sajini Ibrahim,  mlinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania.
 
(Sauti ya Ibrahim)
====================================================
STUDIO. MIDWAYSTING
====================================================
ASSUMPTA: Punde ni makala ambapo tutakuwa mjini Kahama nchini Tanzania kusikia harakati za wazazi kuwazuia watoto kukutana na wenzao kama njia ya kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.
====================================================

3: Dhana potofu kuhusu kinga na tiba ya virusi vya corona
Tangu kuibuka kwa virusi vya corona, COVID-19, duniani kote watu wamekuwa nao wakiibua dhana mbalimbali potofu za kuhusu namna ya kujikinga au kutibu maambukizi ya virusi hivyo. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, kupitia wavuti wake pamoja na mengine, limechapisha baadhi ya dhana hizo potofu na kuzitolea ufafanuzi kama anavyosimulia Flora Nducha
(Taarifa ya Flora Nducha )
WHO inasema wako watu walio na dhana kuwa kujianika katika jua kali au joto la kufikia nyuzi joto 25 kunaweza kuwazuia kupata virusi vya corona. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa linasisitiza kuwa dhana hiyo ni potofu kwani unaweza kupata virusi hivyo bila kujali kama umekaa juani muda mrefu au katika hali ya hewa yenye joto. Bado WHO inasisitiza kuendelea kujilinda kwa kundelea kuosha mikono mara kwa mara, kuepuka kugusa macho, mdomo na pua. 
Watu wengine wamekuwa wakiamini kuwa njia moja ya kujipima mwenyewe kama umeambukizwa virusi vya corona, COVID-19 ni kujaribu kubana pumzi bila kupumua kwa sekunde 10 au zaidi na kwamba usipokohoa au kujisikia vibaya basi hauna virusi vya corona. Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa linasema kuwa hiyo nayo ni dhana potofu kwani njia hiyo si tu haiwezi kukuthibitishia kuwa huna virusi vya corona, bali pia haiwezi kukweleza kuhusu magonjwa mengine ya mapafu. Kwa hivyo WHO inasisitiza njia bora ni kuangalia dalili za ugonjwa huu ambazo kikohozi kikavu, kuchoka na pia kuwa na homa. Ni vema kuwasiliana na wahudumu wa afya pindi unapoona una dalili za namna hiyo ili uweze kupatiwa msaada pamoja na kuwaepusha unaoweza kukutana nao.
 
Aidha WHO inasema wako watu wanaoamini kuwa unywaji wa pombe utawakinga na virusi vya corona, COVID-19, Shirika la afya la Umoja wa Mataifa linawaambia watu hao kuwa pombe si tu haiwezi kukukinga na virusi hivyo, bali pia unywaji wa pombe wa mara kwa mara na uliopita kiwango, unaweza kuwa hatari na kukuweka katika matatizo ya kiafya. 
Na je kuoga maji moto kwaweza kukuepusha na virusi hivi vya corona? La hasha, kwa kawaida joto la mwili wa binadamu hubakia katika nyuzi joto 36.5 hadi nyuzi joto 37 bila kujali joto la maji anayoyaoga. Kimsingi, WHO wanakutahadharisha kuwa kuoga maji ya moto sana kunaweza kuwa hatari kwani unaweza kuunguza Ngozi yako. Kwa hivyo endelea kutumia njia zinazoshauriwa kitaalamu kama vile kunawa mikono mara kwa mara kwa kutumia sabuni na maji tiririka. 
Vipi kuhusu Mbu? Kwani kuna wale wanaoamini kwamba huenda mbu anaweza kuwaambukiza virusi vya corona. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa linasema, hapana. Ingawa unapaswa kuwadhibiti mbu ili wasikuambukize magonjwa mengine kama vile malaria, hadi hivi sasa hakuna ushahidi wowote unaoonesha kuwa wadudu hao wanaweza kusambaza virusi vya corona. Virusi vya corona, COVID-19 vinasambaa kwa pale ambapo maji maji kutoka kwa mtu aliyeathirika yanaposambaa na kuangukia mahali baada ya kupiga chafya au kukohoa au maji maji mengine kutoka mdomoni na katika pua. 
 
Vilevile wapo wale wenye imani kuwa ulaji wa vitunguu saumu kunaweza kuwakinga na COVID-19. WHO inaeleza kuwa ijapokuwa vitunguu saumu ni chakula cha afya lakini hakuna ushahidi wowote kuwa kinaweza kukusaidia kuzuia kuambukizwa virusi vya corona. Kwa hivyo endelea kuwasikiliza wataalamu wa afya
===================================================
STUDIO: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  Na sasa ni makala ambapo Paulina Mpiwa wa redio washirika Huheso FM amepita katika mitaa ya mji wa Kahama nchini Tanzania ili kusikia harakati za wazazi kuwaepusha watoto wao na maambukizi ya virusi vya corona, na kwanza anamuuliza Bi Mariam anafanyaje kumdhibiti mtoto wake?
=================================================
STUDIO: PLAY MAKALA
==================================================== 

ASSUMPTA: Play MUSIC 4 for 5 seconds and hold under
====================================================
ASSUMPTA:  

Asante sana Paulina Mpiwa kwa makala hiyo kutoka Kahama Shinyanga Tanzania..
====================================================
Na sasa ni  mashinani ambapo  Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP nchini Syria Corinne Fleischer anazungumzia hatua walizochukua kuhakikisha kuwa wanufaika wanapata mgao wao wa chakula kwa njia salama zaidi wakati huu ambapo wagonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 wamethibitishwa nchini humo.
====================================================
Studio: Play Mashinani
====================================================
ASSUMPTA: 
Shukrani sana Corinne Fleischer kwa  ujumbe huo.
==================================================
STUDIO: Play Bridge

ASSUMPTA: Na hadi hapo natamatisha jarida letu la leo. Tupatane kesho kwa habari na makala kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa unaweza kupata matangazo na taarifa nyingine na kujifunza Kiswahili kwenye wavuti wetu news.un.org/sw. Msimamizi  wa matangazo ni FLORA NDUCHA na fundi mitambo na mimi ASSUMPTA MASSOI, nasema kwaheri kutoka New York. 

==================================================
TAPE: CLOSING BAND

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
11'42"