Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mradi wa uzazi wa mpango wa UNFPA kisiwani Unguja umeboresha hata mapenzi kati yetu anasema mnufaika wa mradi, Othman Vuai

Mradi wa uzazi wa mpango wa UNFPA kisiwani Unguja umeboresha hata mapenzi kati yetu anasema mnufaika wa mradi, Othman Vuai

Pakua

Na sasa tuelekee Kwarara Unguja, Zanzibar nchini Tanzania ambako shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA limefadhili mradi wa ushirikishaji wa wanaume katika elimu ya afya ya Uzazi.

Afisa Mawasiliano mkuu wa UNFPA Tanzania, Warren Bright katika kukagua miradi hiyo kuangazia miaka 25 ya mafanikio ya mkutano wa kimataifa kuhusu idadi ya watu na maendeleo, ICPD uliofanyika Cairo, Misri mwaka 1994, amezungumza na Mwalimu Othman Maulid Vuai na mkewe Nargis Nassor ambao ni wanufaika wa mradi huo.

Audio Credit
Warren Bright
Audio Duration
2'9"
Photo Credit
World Bank/Binyam Teshome