Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake Morogoro wapata mafunzo ya kunyonyesha vyema watoto wao

Wanawake Morogoro wapata mafunzo ya kunyonyesha vyema watoto wao

Pakua

Kila mwaka Agosti mosi ni mwanzo wa wiki ya unyonyeshaji duniani ikiwa na lengo la kutoa elimu na kuhimiza jamii kuhusu umuhimu wa mtoto kupata maziwa ya mama kwa miezi sita ya mwanzo ya maisha yake.

Kwa kuzingatia hilo mashirika mbali mbali yamechukua jukumu hilo la kuelimisha jamii kuhusu lishe bora hususan kwa watoto wachanga.

Moja ya mashirika hayo ni Save the Children nchiniTanzania ambalo leo limetembelea Kijiji cha Lubeho wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro kwa ajili ya maonyesho kuhusu namna ya kuandaa chakula cha watoto. Akizungumza na John Kabambala wa radio washirika Tanzaniakids FM Afisa mtendaji kata ya Lubeho Rashid Fungafunga ambaye amesema suala la lishe bado ni changamoto kwa kuwa..

 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
2'48"
Photo Credit
UN