Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvutano wa Marekani na Urusi unanitia wasiwasi

Mvutano wa Marekani na Urusi unanitia wasiwasi

Pakua

Mvutano kati ya Urusi na Marekani uliosababisha hata pande mbili hizo kuchukua hatua za kufukuziana maafisa wao wa kibalozi unanitia wasiwasi mkubwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema hayo leo jijini New York, Marekani wakati akijibu swali la mwanahabari baada ya kuzungumza nao kuhusu masuala ya mabadiliko ya tabianchi.

Bwana Guterres amesema hofu yake ni kwamba mwelekeo wa mvutano huo unafanana kidogo na zama za vita baridi kati ya Marekani na Urusi lakini wakazi wa zama hizo pande mbili hizo zilikuwa na udhibiti wa mvutano huo.

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Hivi sasa, tuna pande nyingi ambazo ziko huru na pia zina dhima muhimu kwenye mizozo mingi tunayoshuhudia,na hatari zinazoweza kuibuka ambazo zinafahamika. Kwa upande mwingine wakati wa vita baridi kulikuwa na mfumo wa mawasiliano na udhibiti ulioweza kuepusha kupanuka kwa wigo wa matukio na mizozo.”

Katibu Mkuu amesema mifumo hiyo iliyokuwa na uwezo wa kudhibiti kupanua kwa mizozo ilisambaratishwa kwa sababu watu walidhani kuwa vita baridi imemalizika. Kwa mantiki hiyo amesema..

(Sauti ya Antonio Guterres)

“Naamini ni wakati wa kuchukua tahadhari kwa kuwa na njia thabiti ya mawasiliano na hakikisho la uwezo wa kuepusha hali kudorora. Namini mfumo wa aina hii ni muhimu kuwa nao tena.”

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
1'20"
Photo Credit
UN/Eskinder Debebe