Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usanii wanufaisha wakimbizi nchini Kenya

Usanii wanufaisha wakimbizi nchini Kenya

Licha ya changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa chakula, Kenya inaendelea kuhifadhi wimbi kubwa la wakimbizi wengi kutoka nchi jirani tangu mapema mwaka 1990. Wengi wa wakimbizi hao hawana nafasi za ajira na hivyo hujikuta wakitegemea misaada ya kibinadamu.

Kwa mantiki hiyo, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR Kenya lilizinndua mradi uitwao 'Wasanii Wakimbizi' mwaka 2015, kwa msaada wa wasanii wawili maarufu wa Kenya Henry Ohanga na Victor Ndula.

Wasanii hawa wamewafunza wakimbizi stadi za usanii kupitia warsha mbalimbali na hasa matumizi ya vyombo mbalimbali vya muziki, na hatimaye mradi wa majaribio kutekelezwa katika kambi ya Kakuma kwa hisani ya UNHCR kupitia mshiriki wake nchini Kenya, Film Aid International (FAI).

Tamasha hilo la Muziki pamoja na usanii mbalimbali liliwaleta pamoja washiriki zaidi ya 20 kutoka kambi ya Wakimbizi  ya Kakuma na Dadaab, pamoja na wanamuziki wengine kutoka mji mkuu Nairobi. Katika makala hii, Selina Jerobon anamulika ujasiri wa bendi moja ya wasanii wakimbizi...ungana naye..

Pakua
Audio Credit
Selina Jerobon
Audio Duration
4'4"
Photo Credit
Kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya(Picha ya UM/Evan Schneider)