Mlinda amani wa UM na askari wa Mali wauawa katika shambulio

Mlinda amani wa UM na askari wa Mali wauawa katika shambulio

Pakua

Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema leo asubuhi kumefanyiska shambuliop katika kambi mbili za Douentza jimbo la Mopti Kaskazini mwa Mali na kusababisha vifo na Majeruhi. Na mpango wa Umoja wa mataifa nchini humo MINUSMA umelaani vikali shambulio hilo.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari mjini New York Marekani Farhan Haq amesema..

(SAUTI YAFARHAN HAQ )

"Askari mmoja wa Mali na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa wameuawa katika shambulio hilo, mlinda amani mwingine alijeruhiwa. Mpango wa Umoja wa Mataifa unalaani shambulio hili na tunaungana na wafanyakazi wenzetu kutuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga na kwa serikali yao.”

Washambuliaji wawili wameripotiwa kuuawa katika purukushani hiyo kwenye kambi za MINUSMA za Dountza, mashambulio yaliyoanza saa kumi na moja alifajiri. Washambuliaji wengine walikimbia baada ya askari wa Mali waliokuwa karibu walipokuja kuisaidia MINUSMA.

Photo Credit
Mlinda amani nchini Mali.(Picha:UNIfeed/video capture)