Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuendelea kuzorota kwa hali Sudan Kusini kwatia hofu-UNHCR

Kuendelea kuzorota kwa hali Sudan Kusini kwatia hofu-UNHCR

Pakua

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linatiwa hofu na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama ndani ya Sudan kusini, wakati shambulio la karibuni kabisa kwenye mji wa Pajok jimbo la Equatoria likiwafungisha virago wakimbizi zaidi kwenda kusaka usalama nchi jirani.

Tangu Jumatatu wiki hii wilaya ya Lamwo Uganda imepokea wakimbizi 6000 na mapigano hayo yameripotiwa pia kwenye wilaya za Magwi na Oboo zote zikiwa mpakani na Uganda. Babar Baloch msemaji wa UNHCR anafafanua zaidi

(SAUTI BABAR BALOCH)

"Wafanyakazi wa UNHCR hukokaskazini mwa Ugandahivi sasa wanaendelea kutoa msaada kwa wanawake , watoto, wazee na walemavu wanaoendelea kuwasili. Wakimbizi hao wanahitaji msaada wa kibinadamu kwa dharura, ikiwemo wa chakula, maji, makazi na matibabu. Watu takribani 4000 walikimbia mji wa Pajok pindi shambulio hili la kikatili lilipotokea"

Uganda hivi sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 832,000 kutoka Sudan Kusini.

Photo Credit
Wakimbizi kutoka Sudan kusini waliokimbilia nchi jirani Uganda.(Picha:UNHCR/David Azia)