Syria ni kitovu cha watu kukimbia makwao kimataifa

Syria ni kitovu cha watu kukimbia makwao kimataifa

Pakua

Syria imekuwa kitovu cha kimataifa cha watu wanaokimbia makwao , kwa mujibu wa mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa anayehusika na nasuala ya haki za binadamu.

Wakimbizi wa ndani wana tofauti na wakimbizi wa kawaida , kwa sababu wamelazimika kukimbia makwao lakini wanasalia nchini mwao.

Umoja wa Mataifa unakadiria kwamba hivi sasa kuna wakimbizi wa ndani milioni 40 kote duniani.

Chaloka Beyani ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za wakimbizi wa ndani. Anafafanua ni kwa kiasi gani tatizo la wakimbizi wa ndani ni kubwa Mashariki ya Kati.

(SAUTI YA BEYANI)

“Iraq ina wakimbizi wa ndani milioni 3.5 katika kanda, Syria ina wakimbizi wa ndani milioni 8 ni kitovu cha mgogoro hivi sasa, ukichochewa na vita vya silaha, masuala ya kidini na bila shaka ugaidi.”

Photo Credit
Usambazaji wa msaada wa chakula nchini Syria.(Picha:WFP)