Kuna uhusiano baina ya uhuru wa habari na maendeleo endelevu:UNESCO

Kuna uhusiano baina ya uhuru wa habari na maendeleo endelevu:UNESCO

Pakua

Shirika la sayansi elimu na utamaduni UNESCO limesema maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani yatafanyika Helsink Finland kuanzia Mai 2 hadi Mai 4.

Kauli mbiu yam waka huu ni fursa ya habari na uhuru muhimu, ikitia mkazo katika uhuru wa habari na maendeleo ebndelevu, kulinda uhuru wa habari kutokana na uchujaji wa habari, ufuatiliaji na kuhakikisha usalama wa waandishi wa habari mitandaaoni nan je ya mitandao.

UNESCO inasema uhusiano baina ya uhuru wa habari na maendeleo endelevu umeowanishwa kwa mara ya kwanza mwaka huu , kufuatia kupitishwa mwishoni mwa mwaka 2015 na Umoja wa Mataifa malengo ya maendeleo endelevu SDG’s ifikapo 2030, ambayo yanatambua haja ya kuhakikisha umma unapata fursa ya habari na kulinda uhuru wa msingi kwa kuzingatia sheria za kitaifa na makubaliano ya kimataifa (SDG 16 kipengee cha 10).

Akisistiza hilo mkurugenzi mkuu wa UNESCO Irina Bokova katika ujumbe wake wa maadhimisho ya siku hiyo, amesema umuhimu wa uhuru wa vyombo vya habari katika kuwahabarisha wananchi ni suala nyeti katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu .

Maadhimisho hayo yatahitimishwa kwa semina maalumu Mai 4 itakayotathimini athari za miradi ya maendeleo kuchagiza uhuru wa kujieleza katika ukanda wan chi za Kiarabu ambayo itafadhiliwa na serikali za Finland na Sweden.

Photo Credit
@UNESCO