Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya imehitimisha kampeni ya chanjo ya polio kwa msaada wa UNICEF/WHO

Libya imehitimisha kampeni ya chanjo ya polio kwa msaada wa UNICEF/WHO

Pakua

Kampeni ya kwanza ya kitaifa ya chanjo ya polio imekamilika jana nchini Libya.

Kampeni hiyo ya siku tano inakadiriwa kuwafikia watoto milioni moja chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa kitengo cha taifa cha udhibiti wa magonjwa (NCDC) na msaada kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na lile la afya WHO.

Kabla ya kuanza kampeni UNICEF ilitoa dozi milioni 1.5 za chanjo ya polio nchini humoambazo zimetosheleza kuwachanja watoto karibu milioni 1.2 walio chini ya umri wa miaka 6.

Nalo shirika la afya duniani WHO limegharamia kampeni nzima pamoja na msaada wa kiufundi. Libya imekuwa bila polio tangu mwaka 1991 na kampeni hii ni ya kwanza tangu mwaka 2014.

Photo Credit
Watoto nchni Libya.(Picha:UM/© UNICEF Libya/2011/Tidey)