Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watoto wanaoteswa yaongezeka

Idadi ya watoto wanaoteswa yaongezeka

Pakua

Zaidi ya watoto na vijana barubaru 5,000 wameathirika na mateso mwaka 2015, umesema leo Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kusaidia wahanga wa Mateso UNVFVT, ikilinganishwa na visa 4,000 vilivyoripotiwa mwaka 2014.

Kwenye taarifa iliyotolewa leo, Katibu wa UNVFVT, Laura Dolci-Kanaan, amesema takwimu hizo zinashtua sana, akiongeza kwamba vitendo vya mateso vinarejea na kibaya zaidi, vinakubaliwa na jamii, wakati uhalifu huo haukubaliki.

Ameongeza kwamba ni lazima kuangazia mahitaji maalumu ya watoto walioathirika na mateso.

Mwaka 2015, watu wazima na watoto zaidi ya 57,000 walipewa msaada kupitia mashirika yanayofadhiliwa na UNVFVT, ukiwemo msaada wa kisheria, kisaikolojia na kijamii.

Photo Credit
Watoto miongoni mwa watu wanaoteswa na kufungwa gerezani, hapa ni Liberia. Picha ya UN/Christopher Herwig