Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ayapongeza mataifa ya Amerika ya Kusini na Caribbean (CELAC )

Ban ayapongeza mataifa ya Amerika ya Kusini na Caribbean (CELAC )

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ameyapongeza matifa ya Amerika ya Kusini na Caribbean kwa kuonyesha uongozi shupavu kwenye masuala ya maendeleo endelevu, vita dhidi ya kutokuwepo usawa, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kushughulikia tatizo la usafirishaji na biashara ya mihadarati.

Akizungumza kwenye mkutano wa jumuiya ya mataifa ya Amerika ya Kusini na Caribbean Ban amesema nchi hizo zinazowakilisha watu Zaidi ya milioni 500 ynameonyeshja mshimakano hasa katika kusaidia wahitaji ikiwemo mchango wao mkubwa kwa Haiti, mjanga mengine ya kibinadamu na ukarimu wao wa kujitolea kuwapokea na kuwahifadhi maelfu ya wakimbizi wa Syria.

Ban pia ameyashukuru mataifa hayo kwa juhudi zao za kuunga mkono mchakato wa Amani Colombia ikiwemo kupitisha azimio kwenye mkutano wa mataifa hayo uliofanyika Quito, akisema hatua kwenye mchakato wa Amani ya Colombia ni muhimu kwa ukanda mzima.

Ameyataka mataifa hayo kuendelea kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa ajenda ya mwaka 2030 ya maendeleo endelevu na na mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi.

Photo Credit
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.(Picha:UM/Mark Garten)