Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mauaji ya wanahabari wa Al-Sharqiya, Iraq

UM walaani mauaji ya wanahabari wa Al-Sharqiya, Iraq

Pakua

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini Iraq, Ján Kubiš, amelaani vikali mauaji ya wanahabari wawili wa televisheni ya Al-Sharqiya, katika mkoa wa Diyala nchini Iraq.

Bwana Kubiš amesema mauaji ya Saif Talal na Hassan Al-Anbaki wakiwa wanafanya kazi yao ya kutoa habari kuhusu matukio ya Diyala ni kitendo cha uovu na uoga kilichotekelezwa na watu wasiotaka ukweli usemwe.

Ametoa wito kwa mamlaka ziwakabili hima waliotenda kitendo hicho, na kuwafikisha mbele ya sheria, pamoja na kufanya kila liwezekanalo ili kuwalinda wanahabari wanapofanya kazi yao.

Ametuma rambirambi zake kwa familia, rafiki na wafanyakazi wenza wa wahanga hao.

Photo Credit
Mwakilishi wa Katibu Mkuu na Mkuu wa UNAMA, Ján Kubiš