Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi ikielekea uchaguzi mkuu , Umoja wa Mataifa wataka utulivu

Burundi ikielekea uchaguzi mkuu , Umoja wa Mataifa wataka utulivu

Pakua

Taifa la Burundi lilioko Afrika Mashariki , linajiandaa kwa uchaguzi mkuu mwezi mei mwaka huu.  Hata hivyo joto la kisiasa limeanza kupanda miezi mitatu kabla ya zoezi hilo. Shughuli ya kuwaorodhesha wapiga kura katika daftari la wapiga kura, imemalizika chini ya mvutano mkubwa kati ya serikali na upinzani.Baada ya kufungwa rasmi kwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi BNUB mwanzoni mwa mwaka huu, Umoja huo umeunda tume ya uangalizi wa uchaguzi na hivyo kutoa wito wa kufanyika uchaguzi  huru  na wa haki ili kulinusuru taifa na machafuko kama yale yaliyowahi kutokea nchini humo miaka iliyopita.

Mjumbe maalumu  wa katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kwenye ukanda wa maziwa makuu Said Djinit amesema ufanisi wa uchaguzi huo utakuwa ni njia ya kuimarisha demokrasi na  utulivu nchini humo. Je nini kinaendelea na nini kinafanyika ili kufanikisha hilo? kutoka Bujumbura, muandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani Kibuga ametuandalia makala ifuatayo.

Photo Credit
Upigaji kura nchini Burundi(Picha ya UM/Martine Perret)