Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Redio ni chombo adhimu kwa jamii kaskazini mashariki mwa Kenya

Redio ni chombo adhimu kwa jamii kaskazini mashariki mwa Kenya

Pakua

Umuhimu wa redio katika jamii mbalimbali ni dhahiri ikizingatiwa kwamba chombo hiki kinatumika kwa mawasiliano na maswala mbalimbali ya kijamii. Pia redio ni daraja ya mawasiliano kati ya wananchi na serikali, hususan katika maeneo ya pembezoni. Nchini Kenya baadhi ya jamii za pembezoni zimekuwa zikitengwa lakini sasa uwepo wa radio umefungua mlango wa mawasiliano. Basi ungana na Geoffrey Onditi wa redio washirika KBC, katika makala hii.

Photo Credit
Bwana Hassan alikimbia Somalia 1994 na anaishi kwenye kambi ya Dadaab.(Picha ya UNHCR / S. Ostermann)