Skip to main content

Umoja, Mshikamano wa Pamoja ndiyo Njia Bora ya Kutanzua mzozo wa Guinea-Bissau

Umoja, Mshikamano wa Pamoja ndiyo Njia Bora ya Kutanzua mzozo wa Guinea-Bissau

Pakua

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa amependekeza hatua zinazopaswa kupitiwa ili kutafutia majawabu mzozo wa kisiasa uliolikumba taifa la Guinea-Bissau lililopo katika pembe ya Afrika Magharibi ambalo hivi karibuni lilishuhudia mapinduzi ya kijeshi.

Taifa hilo hata hivyo linahistoria ya kukumbwa na matukio ya wanajeshi kupoka madaraka tangu lilipojipatia uhuru wake mwaka 1974 toka wa Ureno.

Mwanadiplomasia wa Umoja wa Mataifa anayehusika na ujenzi wa amani Joseph Mutaboba amesema kuna haja ya viongozi wa taifa hilo kuanzisha shabaha ya kukaa meza moja na kujadilia kurejesha mfumo wa kikatiba haraka iwezekanavyo.

Akiwasilisha hali jumla ya mambo kwenye kikao cha baraza la usalama, Bwana Mutaboba ameonya juu ya kuzorota kwa taasisi za maamuzi ambazo zimevurugwa kutokana na matukio ya mara kwa mara ya kukosekana utengamao.

Akizungumza na Maha Fayek wa Radio ya Umoja wa Mataifa, Bwana Mutaboba amesema kuwa hali ya kiuchumu na ya kujamii nchini humo, imeendelea kuzorota tangu mapinduzi ya kijeshi mwezi Aprili, na kutia hofu ya hali ya kibinadamu.