Wahamiaji waliorejeshwa Sudan Kusini kutoka Sudan wanasema asante IOM
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM nchini Sudan kusini kwa kushirikiana na wadau wake wa masuala ya kibinadamu wanafanya kazi usiku na mchana kusaidia wakimbizi walioko Sudan wanaotaka kurejea nyumbani nchini Sudan Kusini na kuwaunganisha tena na familia zao.