Balozi Affey mjumbe maalum kuhusu wakimbizi Somalia
Hii leo Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filipo Grandi amemteua Balozi Mohamed Abdi Affey kuwa mjumbe wake maalum kwa masuala ya wakimbizi huko Somalia.
Hii leo Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Filipo Grandi amemteua Balozi Mohamed Abdi Affey kuwa mjumbe wake maalum kwa masuala ya wakimbizi huko Somalia.
Mustakhbali wa kijamii na kisiasa kwa mataifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Burundi kwenye ukanda wa maziwa makuu, uko mikononi mwa nchi husika na wadau wote wa ukanda mzima, Jumuiya ya Afrika Mashariki na jumuiya ya kimataifa.
Tarehe 29 Septemba kila mwaka dunia huadhimisha siku ya moyo. Siku ambayo wadau wa masuala ya afya wakiratibiwa na shirika la afya ulimwenguni WHO hutumia kama jukwaa la kuhamasisha kuhusu magonjwa ya moyo.
Hatimaye leo Ijumaa kikao cha 33 cha baraza la haki za binadamu kimefunga pazia mjini Geneva Uswiss, kwa wito kwa nchi wanachama kuchukua hatua dhidi ya ukatili na uwajibikaji kwa wahusika.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameunda bodi itakayochunguza tukio la kushambuliwa kwa msafara wa misaada ya kibinadamu huko Urum al-Kubra nchini Syria.
Mwimbaji nyota wa kipalestina, Mohamed Assaf ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA. Yeye hutumia kipaji chake cha kuimba ili kuinua matumaini miongoni mwa wale ambao hata leo yao ni ndoto, sembuse kesho.
Wiki hii tunaangazia neno “PETE” na mchambuzi wetu ni Onni Sigalla Mhariri Mwandamizi, katika Baraza la Kiswahili la Taifa, BAKITA, nchini Tanzania.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na wadau wake wamekamilisha kampeni ya siku sita ya kufikisha huduma za afya na lishe kwa wahitaji nchini Yemen.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya duniani, WHO Dkt, Margaret Chan amepazia sauti yake wito wa kuwepo kwa njia salama za kuhamisha watu wanaojeruhiwa na mashambulizi yanayoendelea nchini Syria, sambamba na kufikisha vifaa vya tiba.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNICEF linawekeza katika kuhakikisha ulinzi wa watoto nchini Tanzania kwa kuboresha mifumo ya kisheria na sera ili kuwahusisha wadau muhimu katika jukumu hilo.