Mradi wa maji waleta nuru kambi ya Dadaab
Kambi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya inahifadhi wakimbizi kutoka Somalia. Kambi hii inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko kambi zote za wakimbizi duniani ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya Laki Nne na Nusu. Uhaba wa maji umekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo.