Kikao kuhusu Somalia chakamilika mjini Copenhagen
Kikao cha 20 cha kimataifa cha kundi la Somalia, kimekamilisha mkutano wa siku mbili mjini Copenhagen, nchini Denmark. Mkutano huu umezungumzia mipango wa kumaliza kipindi cha mpito cha serikali ya mpito ya Somalia ifikapo Agosti 12.