Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kenya imeandaa mikakati kukabili NCD's:Mugo

Kenya imeandaa mikakati kukabili NCD's:Mugo

Pakua

Serikali ya Kenya imesema licha ya changamoto za fedha, vifaa na wataalamu imejiandaa na kuweka mikakati ya kitaifa kukabiliana na maradhi yasiyo ya kuambukiza.

Kwa mujibu wa waziri wa afya wa nchi hiyo Bi Beth Mugo magonjwa kama saratani, kisukari, magonjwa ya moyo na matatizo ya kupumua ni magonjwa ya gharama kubwa kwa upande wa matibabu na wananchi, na serikali pekee hawawezi kukabilia bali mshikamano wa kimataifa unahitajika hasa katika kusaidia nchi masikini.

Akizungumza na mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa Flora Nducha waziri Mugo amesema pia tabia za watu kuhusu vyakula na maisha yao lazima zibadilike. Wasikilize.

(MAHOJIANO NA WAZIRI BETH MUGO)