Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

26 AGOSTI 2024

26 AGOSTI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunamulika kupelekwa kwa chanjo dhidi ya polio huko Gaza; mkimbizi wa Burundi aliyerejea nyumbani kutoka Tanzania ainuliwa kiuchumi; makala ni mkimbizi wa Sudan aliyeko ugenini naye awezeshwa kijasiriamali na mashinani tunabisha hodi nchini Rwanda kumulika usawa wa kijinsia kwenye michezo.

  1. Hatimaye shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linapeleka Gaza huko Mashairki ya Kati dozi milioni 1.2 za chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio aina ya 2, wakati huu ambapo ugonjwa huo hatari umethibitishwa kuweko eneo hilo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
  2. Kwa wakimbizi, kurejea nyumbani ni jambo moja na kuanza upya ni jambo lingine. Wengi wao hawana chaguo lingine isipokuwa kuanza maisha yao upya. Mkoani Makamba, nchini Burundi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kushirikiana na Shirika la Ushirikiano wa Kimataifa la Korea (KOICA) wanawawezesha waliorejea nyumbani kujijenga upya na kwa tija. Miongoni mwao ni Emelyne Kabura kama anavyosimulia Bosco Cosmas
  3. Katika makala Evarist Mapesa anatuletea simulizi ya mkimbizi wa Sudan ambaye sasa anaishi Sudan Kusini. Baada ya kupitia madhila lukuki amewezeshwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa na sasa anajishughulisha na ujasiriamali.
  4. Na sasa ni mashinani  Christelle Umuhoza, Mkurugenzi wa Programu wa Rwanda katika shirika la Shooting Touch, kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO nchini humo, anaeleza umuhimu wa michezo katika kuondoa vikwazo vya kijinsia.
Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Sauti
9'43"