Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

23 MEI 2024

23 MEI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada ka kina inayotupeleka huko wilaya ya Abyei iliyoko kati ya mpaka wa Sudan Kusini na Sudan lilifanyika shambulizi la kuvizia wakati gari la Umoja wa Mataifa lilipokuwa likisafirisha raia waliojeruhiwa, ambalo lilisababisha kifo cha mlinda amani. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa methali “Kanga hazai ugenini.”  

  1. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambalo ni tundu kati ya njia ya uzazi na kibofu cha mkojo, inayosababishwa mara nyingi na uchungu wa muda mrefu wakati wa kuelekea kujifungua, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ya uzazi na masuala ya kijinsia UNFPA Natalia Kanem amesema Fistula ya uzazi ni matokeo ya kusikitisha ya kushindwa kulinda haki za uzazi za wanawake na wasichana walio katika mazingira magumu zaidi na ni lazima itokomezwe kwa watu wote. 
  2. Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Palestina Matthew Hollingworth ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kwamba maelfu ya familia zinazokimbia Rafah zinajikuta zikiwa na uhaba wa chakula na maji safi.
  3. Mvua nyingi zaidi kuliko kawaida inatabiriwa katika maeneo mengi ya Pembe ya Afrika kuanzia mwezi Juni hadi Septemba mwaka huu. Maeneo yatakayotarajiwa kuwa na hali hiyo ni Djibouti, Eritrea, kaskazini na katikati mwa Ethiopia, magharibi na pwani ya Kenya, sehemu kubwa ya Uganda, Sudan Kusini, na Sudan.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “Kanga hazai ugenini.”

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
10'36"