Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

04 APRILI 2024

04 APRILI 2024

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia ujumuishwaji wa wanawake katika masuala ya kifedha kwa lengo la kutimiza lengo la Umoja wa Mataifa la usawa wa kijinsia katika Nyanja zote. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na katika kujifunza kiswahili tunakuletea ufafanuzi na tofauti ya maneno “Adhuhuri na Alasiri”.

  1. Leo ni siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini na msaada wa kuchukua hatua dhidi ya mabomu hayo. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mabomu, vilipuzi na vifaa vingine vya mlipuko vinaendelea kuua na kujeruhi watu katika maeneo mengi yenye changamoto kubwa za migogoro duniani na matokeo yake vifaa hivyo vya mlipuko, kwa wastani hukatili maisha ya mtu mmoja kila saa, na waathirika wakubwa wakiwa ni watoto.
  2. Mratibu wa Misaada ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Palestina linalokaliwa kwa mabavu, Jamie McGoldrick anaelekea Gaza leo. Umoja wa Mataifa unaeleza  kuwa mapigano makali kati ya wanajeshi wa Israel na makundi yenye silaha ya Palestina yanaendelea kuripotiwa katika sehemu kubwa ya Ukanda wa Gaza. 
  3. Mfumo wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni (WHO) wa Ufuatiliaji kuhusu Mashambulizi dhidi ya Huduma za Afya (SSA) wameeleza kuwa inatia wasiwasi kwamba nchini Ukraine wahudumu wa afya katika gari za wagonjwa na wafanyakazi wengine wanaotoa huduma za usafiri wa afya wanakabiliwa na hatari ya kujeruhiwa na kifo mara 3 zaidi ya ile ya wafanyakazi wengine wa huduma za afya.
  4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia tofauti ya “Adhuhuri na Alasiri.”.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
11'7"