IOM yatoa dola elfu 75 kusaidia waathirika wa mafuriko Lao
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, limetoa dola elfu 75 kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyosababishwa na kupasuka kwa kingo za bwawa la maji la kuzalisha umeme la Xenamnoy huko jimbo la Champassak kusini magharibi mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Lao .
Kwa mujibu wa mamlaka za Lao, kupasuka kwa kingo hizo na mafuriko kulichochewa na mvua kali zitokanazo na kimbunga Son-Tinh kilichokumba ukanda huo na kuathiri zaidi ya majimbo 11 na zaidi ya watu 16,256 nchini humo.
Hali ni mbaya zaidi katika vijiji 13 vya wilaya ya Sanamxay, ambako watu 6,351 wameathirika.
IOM inasema watu 3,060 wamepoteza makazi na sasa wamehamishiwa katika makazi ya muda ya dharura.
Mkuu wa IOM nchini Lao Misato Yuasa amesema mpaka sasa watu 26 wameripotiwa kufariki dunia huku wengine 131 hawajulikani walipo na zaidi ya yote..
“ IOM sasa inatumia ujuzi wake wa kimataifa katika kubabiliana na dharura katika kuisaidia serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu Lao, kama wanachama wapya zaidi ya yote kukabiliana na hali ya janga hili kubwa. Lakini pia tumejitolea kuwasaidia watu hawa hapo baadaye mpaka tuhakikishe maisha yao yanarejea na kwa kuwafikia wafadhili wa kimataifa”.
IOM imewapeleka nchini Lao wataalamu wake wa kiufundi kwenye masuala ya ujenzi wa makazi ya dharura, usimamizi wa makazi, uhamiaji na masuala ya vifaa. Wataalamu hao wanatoka ofisi ya IOM ya kanda ya Asia-Pasifiki iliyoko Bangkok, Thailand.
Misaada ya dharura ya uokoaji katika majanga inapangwa kwa sekta ambapo IOM inashirikiana na wataalam wengine kuoka UN Habitat na Wizara ya Ujenzi wa Umma na Nyumba. Pia na makundi ya wataalamu wa afya na maji kutoka WHO na huduma za maji na kujifasi au WASH kutoka UNICEF.
IOM, ilianza operesheni zake huko Lao mwaka 2002 na mwezi Juni mwaka 2018 nchi hiyo ilijiunga na shirika hilo ikiwa ni mwanachama wake wa 171.
Tags: IOM, LAO, UNHabitat, UNICEF