Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres atoa wito wa mageuzi katika ufadhili wa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António  Guteres akihutubia wakati wa kufungwa kwa mkutano wa Jukwaa la kimataifa la biashara la nchi zinazoendelea za visiwa vidogo, SIDS huko Antigua na Barbuda
UN Photo/Eskinder Debebe

Ukuaji wa Kiuchumi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ; António Guterres ameangazia uwezekano wa nchi za Visiwa Vidogo zinazoendelea kukabiliwa na majanga ya tabianchi na kifedha na hivyo akatoa wito wa msamaha wa madeni, mabadiliko ya taratibu za utoaji mikopo na kujumuishwa katika taasisi za fedha za kimataifa ili kusaidia nchi hizi zilizoathirika kwa kiasi kikubwa.