Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za visiwa vidogo zakutana Antigua na Barbuda kupanga njia mpya ya ustawi endelevu

Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo zinazoendelea  (SIDS4).
UN Photo
Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo zinazoendelea (SIDS4).

Nchi za visiwa vidogo zakutana Antigua na Barbuda kupanga njia mpya ya ustawi endelevu

Ukuaji wa Kiuchumi

Mkutano wa nne wa Kimataifa wa Nchi za Visiwa Vidogo Zinazoendelea (SIDS4) umeanza leo katika mji mkuu wa Antigua na Barbuda, St. John ili kutoa mpango wa utekelezaji wa kijasiri na wa mageuzi ili kusaidia SIDS kujenga mnepo, kukabiliana na changamoto kubwa zaidi duniani na kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

 

Viongozi wa dunia, pamoja na wawakilishi kutoka sekta binafsi, mashirika ya kiraia, wasomi na vijana, wamekusanyika katika Mkutano huo ili masuala muhimu yanayoathiri mustakabali wa SIDS. Chini ya mada "Kuandaa kozi kuelekea kusonga mbele", Kola siku nne (27-30 Mei) litaonyesha ubunifu mpya na kubuni masuluhisho ya vitendo ili changamoto muhimu za SIDS zinazoendeshwa na dharura ya hali ya hewa, kuongezeka kwa madeni na majadiliano ya afya .

Guterres na ajenda

Mkutano huo utapitisha Ajenda ya Antigua na Barbuda kwa SIDS (ABAS) – Tamko Lililohuishwa kwa Ustawi wenye mnepo, ambalo linaweka wazi matarajio ya maendeleo endelevu ya visiwa vidogo katika kipindi cha miaka 10 ijayo na usaidizi unaohitajika kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ili kuyafikia.

"Ajenda mpya ya Antigua na Barbuda kwa Nchi Zinazoendelea za Visiwa Vidogo inaeleza hatua za kufikia ustawi thabiti kwa ushirikiano na jumuiya ya kimataifa," Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema.

Guterres ameongeza kwa kuziomba serikali za SIDS “kuunga mkono maneno haya kwa uwekezaji wa ujasiri na ushirikishwaji endelevu katika sekta zote za maendeleo endelevu. Lakini SIDS haziwezi kufanya hivi peke yake. Jumuiya ya kimataifa ina wajibu wa kuunga mkono Mataifa yanayoendelea ya Visiwa Vidogo yakiongozwa na nchi ambazo zina wajibu mkubwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili.”

Pia Guterres ameziambia nchi zinazoendele za visiwa vidogo kwamba, “Umoja wa Mataifa unasimama nanyi katika kuthibitisha matarajio ya SIDS: kusitisha na kupunguza athari mbaya za janga la tabianchi; kujenga uchumi imara; kukuza jamii salama, zenye afya na ustawi; kufikia usalama wa maji, chakula na nishati; kuhifadhi bioanuwai; na kulinda na kutumia kwa njia endelevu bahari na rasilimali zake.”

Akirejelea hili, Li Junhua, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa Masuala ya Kiuchumi na Kijamii ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Mkutano wa SIDS4 amesisitiza: “Ajenda inaeleza simulizi ya SIDS, safari yao, matumaini na changamoto zao. Lakini muhimu zaidi, Ajenda inaionesha jumuiya ya kimataifa hatua mahususi ambazo Nchi Wanachama, washirika wa maendeleo, taasisi za fedha, mfumo wa Umoja wa Mataifa na wadau wanapaswa kuchukua ili kutoa na kufuatilia matarajio ya SIDS ya ustawi na mustakabali endelevu kwa watu wao na sayari yetu.”

Li Junhua ameongeza kusisitiza kwamba kwa pamoja, watatumia mkutano huu kama kichocheo cha kujenga na kufanya upya ushirikiano, mbinu za ubunifu za ufadhili na hatua madhubuti zitakazosaidia mataifa haya ya ajabu ya visiwa na watu wao kujenga mustakabali thabiti na endelevu ambao hauachi kisiwa chochote nyuma.