Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Israel yakumbushwa kutekeleza wajibu wake wakulinda watu wenye ulemavu

Watu wa Gaza wanaendelea kuhamishwa kwa nguvu. Tangu mashambulizi ya kijeshi ya Rafah kuanza Mei 6, zaidi ya watu 630,000 wamelazimika kukimbia eneo hilo.
© UNRWA
Watu wa Gaza wanaendelea kuhamishwa kwa nguvu. Tangu mashambulizi ya kijeshi ya Rafah kuanza Mei 6, zaidi ya watu 630,000 wamelazimika kukimbia eneo hilo.

Israel yakumbushwa kutekeleza wajibu wake wakulinda watu wenye ulemavu

Haki za binadamu

Kamati ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Watu Wenye Ulemavu hii leo imeeleza kuwa watu wenye ulemavu walioko Gaza wapo kwenye hali ngumu na watakuwa wa kwanza kuuawa kutokana na fursa chache za kuwawezesha kukimbia maeneo ambayo Israel inatangaza wanatakiwa kuondoka kabla haijafanya mashamulizi. 

 

Katika taarifa yao iliyotolewa jijini Geneva Uswisi kamati hiyo imeitaka Israel ikiwa ni mamlaka inayokalia eneo la Gaza kwa mabavu na pia ikiwa ni mtia saini wa mkataba wa Haki za watu wenye ulemavu kutimiza wajibu wake chini ya kifungu cha 11 na kuchukua hatua zote zinazohitaji ili kuhakikisha wanatoa ilinzi na usalama kwa watu wenye ulemavu wanaokuwa katika maeneo ya hatari ikiwemo maeneo yenye migogoro ya silaha. 

Kamati hiyo imetoa mifano ya masahibu mbalimbali yaliyo wakumba watu wenye ulemavu Gaza tangu kuzuka kwa mapigano Oktoba 7, 2023 pamoja na idadi kubwa ya watu wanaopata ulemavu kutokana na vita vinavyoendelea na kueleza kuwa hali yao ya ulemavu mbali ya kuwafanya washindwe kuhama hama kama wanavyotakuiwa na amri zinazotolewa na Israel lakini pia hata pale wanapokuwa maeneo waliyohamishwa maisha yao yanashindwa kuendelea kutokana na kutokuwepo kwa miundombinu rafiki kwa walemavu pamoja na vifaa vya kuwasaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

“Hali ya kuzingirwa kwa wananachi wa Gaza imesababisha shida ya upatikanaji wa chakula na watu wenye ulemavu wanapata vikwazo vya kimwili vya kufika katika maeneo yanayotoa msaada wa chakula au hawana vifaa vya kuwasaidia kufika katika maeneo hayo” imesema kamati hiyo. 

Si tu suala la chakula hata matibabu yao pia ni changamoto. Kamati hiyo imeeleza “kusikitishwa sana na ukosefu wa huduma za matibabu na dawa zinazohitajika kwa ajili ya matibabu ya magonjwa sugu kwa watu wenye ulemavu, ukosefu wa msaada wa kisaikolojia na hatari kubwa ya vifo wakati wa misako na mashambulizi hospitalini, na umwagaji hewani wa kemikali ya  fosforasi nyeupe na sumu ambayo inaeleza kusababisha hatari kubwa za kupata kasoro zaidi.”

 

Mifano ya waliodhurika

Baba mwenye upofu

Kamati hiyo imetoa mifano ya walemavu mbalimbali ambao wameteseka au/ na kupoteza maisha kutokana na Israel kutotimiza wajibu wake kama mwanachama wa mkataba wa kulinda watu wenye ulemavu ambapo moja ya waathirika ni mwanaharakati wa asasi ya kiraia waliyemtambulisha kwa jina ya Y.M ambaye alikuwa na tatizo la upofu ambaye aliuawa akiwa nyumbani kwake Desemba 7, 2023 baada ya shambulio la bomu. 

Baba huyu ambaye ana upofu hakuweza kufahamu kuhusu agizo la kutakiwa kuondoka katika eneo hilo kwa wakati na hivyo alifariki wakati wa shambulio hilo. Ameacha watoto wa miaka 2.3,8 na 10. Laiti kama angeweza kupata taarifa kwa wakati pengine angeweza kuondoka katika eneo hilo. 

Binti aliyepooza mgongo,

Binti huyu mwenye umri wa miaka 14 mkimbia wa ndani katika eneo la Mashariki mwa Gaza anategemea kiti cha magurudumu matatu ili aweze kutoka sehemu moja kwenda nyingine, wakati wa mashambulizi kiti chake hicho kiliharibiwa na makombora ya kijeshi. 

Ilipokuja amri ya jeshi la Israel ya kuwataka kuondoka familia yake ililazimika kumbeba. Safari ilikuwa ya maumivu na walipokuwa njiani binti huyo alimwambie mzazi wake “Mama inatosha. Niache hapa, na nyie endeleeni kukimbia.” Aliendelea kuweweseka na maonyo yaliyokuwa yakitolewa na majeshi ya Israel huko Rafah na bado angali katika hatari ya kutakiwa tena kuondoka ilihali hana kifaa cha kumsaidia kutembea. 

Watoto wenye ulemavu wa akili,

Nao pia wapo katika wakati mgumu sana kutokana na hali ya kivita huko Gaza. Mmoja wao ni mtoto wa kiume aitwaye Amir ambaye pamoja familia yake walilazimika kukimbia kutika Khan Younis na hivyo kukosa fursa ya masomo na matibabu ya hali yake. “Hali ya Amir imekuwa ikizorota, na amekuwa na wasiwasi sana tangu walipohamia kwenye hema.”

Hali ya Amir na msichana mwenye umri wa miaka 14 imeonesha dhahiri shahiri dhiki inayoendelea ya kisaikolojia na kiwewe wanachopata watoto wenye ulemavu huko Gaza. 

Kabla ya Oktoba 7, 2023, 21% ya familia huko Gaza ziliripoti kuwa na angalau mwana familia mmoja wenye ulemavu, na kulikuwa na watu 58,000 wenye ulemavu waliosajiliwa kwenye kazidata ya Palestina. Tnagu kuanza kwa mapigano Oktoba 7 zaidi ya watoto 1,000 wamekatwa viungo. 

Idadi hii, hatahivyo inaweza kuwa kubwa zaidi kufuatia miezi saba ya mapigano. Inasalia kuwa nivigumu kupata takwimu za uhakika na taarifa za watu wenye ulemavu.