Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UDADAVUZI: Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ni nini?

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC mjini The Hague Uholanzi
UN Photo/Rick Bajornas
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya ICC mjini The Hague Uholanzi

UDADAVUZI: Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC ni nini?

Sheria na Kuzuia Uhalifu

Inahukumu kesi za uhalifu mkubwa zaidi, inahakikisha waathiriwa wanapata haki, inaendesha kesi kwa haki na kumsaidia mahakama za kitaifa ni miongoni mwa majukumu muhimu ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC.

ICC iliyoanzishwa mwaka 2002 na yenye makao yake The Hague Uholanzi , ni mahakama ya jinai ambayo inaweza kuleta kesi dhidi ya watu binafsi kwa uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Hatua yake mpya kabisa ni Jumatatu 20 Mei ambapo imewasilisha ombi la hati za kukamatwa kwa Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant na viongozi watatu wa Hamas, mamlaka kuu huko Gaza.

Hati hizo ambazo sasa lazima ziidhinishwe rasmi na majaji wa ICC zinahusiana na madai ya uhalifu wa kivita unaotokana na vita ya miezi saba sasa huko Gaza iliyochochewa na mashambulizi yanayoongozwa na Hamas nchini Israel.

Haya ni mambo matano kuhusu ICC na jinsi inavyosaidia kujenga ulimwengu wenye haki zaidi.

Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu.
UN News
Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu wa Israel akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha 78 cha Baraza Kuu.

1. Kuhukumu uhalifu mkubwa zaidi

ICC iliundwa kwa kuzingatia "mamilioni ya watoto, wanawake na wanaume" ambao wamekuwa waathirika wa ukatili usiofikirika ambao unashtua sana dhamira ya ubinadamu".

Ni mahakama ya kwanza kimataifa ya kudumu, yenye msingi wa mkataba wa kimataifa kuchunguza na kuwafungulia mashtaka wahalifu wa uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita, mauaji ya kimbari na uhalifu wa uchokozi.

Mahakama hiyo imefanikiwa kuwashtaki watu binafsi kwa uhalifu wa kivita waliotenda katika iliyokuwa Yugoslavia, ikiwa ni pamoja na huko Srebrenica, na imesuluhisha kesi zenye umuhimu kwa haki ya kimataifa, kutoa mwanga juu ya uhalifu wa kutumia askari watoto, uharibifu wa turathi za kitamaduni, unyanyasaji wa kijinsia  na kingono au mashambulizi ya watu, raia wasio na hatia 

Kupitia hukumu zake katika kesi za mfano, mahakama hiyo inajenga sheria za kesi zenye mamlaka hatua kwa hatua.

Mahakama imechunguza baadhi ya migogoro mikubwa zaidi duniani, ikiwa ni pamoja na Darfur, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Gaza, Georgia na Ukraine. 

Kwa sasa inaendesha vikao vya hadhara, ikiwa na kesi 31 kwenye orodha yake ya hati , na orodha yake ya hati inamjumuisha Rais wa Urusi Vladimir Putin na watu binafsi nchini Libya.

Hata hivyo, kutoa hati na kuwakamata washukiwa ni changamoto. Mahakama haina polisi wa kutekeleza vibali vyake vya watu kukamatwa na inategemea nchi wanachama kutekeleza maagizo yake. Wengi wa watu walioshtakiwa na mahakama hiyo wametoka nchi za Kiafrika.

Mtoto aliye na utapiamlo mkali na upungufu wa maji mwilini anatibiwa katika hospitali ya shambani kusini mwa Gaza mnamo Aprili 2024.
© WHO
Mtoto aliye na utapiamlo mkali na upungufu wa maji mwilini anatibiwa katika hospitali ya shambani kusini mwa Gaza mnamo Aprili 2024.

2. Kuhusisha waathirika

Siku yoyote ile, ukitazama kesi za ICC, kuna uwezekano utasikia ushuhuda wa mashahidi au kusikiliza wakili anayewakilisha maoni ya waathiriwa mahakamani. Ushahidi wao na maelezo yao ni muhimu kwa mchakato wa mahakama.

Mahakama haijaribu tu kuwaadhibu wale waliohusika na uhalifu mkubwa zaidi, lakini pia inahakikisha kwamba sauti za waathirika zinasikika. Waathiriwa ni wale ambao wamepata madhara kutokana na kutendeka kwa uhalifu wowote ndani ya mamlaka ya mahakama.

Waathirika hushiriki katika hatua zote za kesi za mahakama ya ICC. Zaidi ya waathirika 10,000 wa dhuluma wameshiriki katika kesi, na mahakama inadumisha mawasiliano ya moja kwa moja na jamii zilizoathiriwa na uhalifu ndani ya mamlaka yake kupitia programu za kuwafikia.

Mahakama pia inataka kulinda usalama na uadilifu wa kimwili na kisaikolojia wa waathirika na mashahidi. Ingawa waathirika hawawezi kuleta kesi, wanaweza kuleta taarifa kwa Mwendesha Mashtaka, ikiwa ni pamoja na kuamua kama watafungua uchunguzi.

Wakfu wa ICC kwa ajili ya waathirika kwa sasa unafanya maagizo ya kwanza ya Mahakama kuhusu ulipaji wa fikia kuwa s ndoto bali hali halisi, ikiwa ni pamoja na madai ya fidia kwa waathirika na familia zao nchini DRC. Kupitia programu zake za usaidizi, wakfu huo pia umetoa msaada wa kimwili, kisaikolojia na kijamii na kiuchumi kwa zaidi ya waathirika 450,000.

Mwendesha Mashtaka wa ICC Karim Khan akitembelea eneo la kutupia taka huko Tarhunah, Libya, ambako idadi ya makaburi ya halaiki yamegunduliwa.
ICC
Mwendesha Mashtaka wa ICC Karim Khan akitembelea eneo la kutupia taka huko Tarhunah, Libya, ambako idadi ya makaburi ya halaiki yamegunduliwa.

3. Kuhakikisha haki katika kesi 

Washtakiwa wote wanachukuliwa kuwa hawana hatia hadi itakapothibitishwa kuwa na hatia bila shaka yoyote mbele ya ICC. Kila mshtakiwa ana haki ya kushtakiwa na kesi kusikizwa na bila upendeleo.

Katika mahakama ya ICC, washukiwa na watuhumiwa wana haki muhimu, zikijumuisha: kufahamishwa mashtaka, kuwa na muda na nyenzo za kutosha kuandaa utetezi wao, kuhukumiwa bila kuchelewa, kwa uhuru kuchagua mwanasheria, na kupokea ushahidi wa udhuru kutoka kwa Mwendesha Mashtaka.

Miongoni mwa haki hizo ni haki ya kufuata mwenendo wa kesi katika lugha ambayo mtuhumiwa anaielewa kikamilifu. Hii imesababisha mahakama kuajiri wakalimani na wafasiri maalumu katika lugha zaidi ya 40, wakati mwingine kutumia, wakati huo huo, lugha nne wakati wa kusikilizwa kwa kesi moja.

Katika miaka yake 20 ya kwanza, washiriki walikabiliwa na aina mbalimbali za changamoto kubwa na za kiutaratibu, kuwa maili nying mbali na matukio ya uhalifu. Kwa kuongezea, uhalifu unaoshtakiwa na ICC ni wa asili maalum na mara nyingi uhalifu mkubwa unaohitaji kiwango muhimu cha ushahidi na juhudi nyingi ili kuhakikisha usalama wa mashahidi. Kesi ni ngumu, na kuna mambo mengi ambayo yanahitaji kutatuliwa nyuma ya pazia wakati wa kesi.

Dorika, manusura wa ubakaji katika vita vya Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Finbarr O’Reilly
Dorika, manusura wa ubakaji katika vita vya Kivu Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

4. Kuzisaidia mahakama za kitaifa

Mahakama ya ICC haichukui nafasi ya mahakama za kitaifa. Ni mahakama ya chaguo la mwisho. Mataifa yana jukumu la msingi la kuchunguza, kujaribu na kuwaadhibu wahalifu wa uhalifu mbaya zaidi. Mahakama ya ICC itaingilia tu ikiwa nchi ambayo uhalifu mkubwa chini ya mamlaka ya mahakama umetendwa haiko tayari au haiwezi kushughulikia kwa dhati uhalifu huo.

Machafuko makubwa yanaongezeka kwa kasi duniani kote. Rasilimali za mahakama zinabsalia kuwa ndogo, na zinaweza tu kushughulikia idadi ndogo ya kesi kwa wakati mmoja. Mahakama inafanya kazi bega kwa bega na mahakama za kitaifa na kimataifa.

5. Kujenga uungwaji mkono zaidi wa haki

Kwa kuungwa mkono na mataifa wanachama zaidi ya 120, kutoka mabara yote, ICC imejiimarisha kama taasisi ya kudumu na huru ya kimahakama.

Lakini, tofauti na mifumo ya mahakama ya kitaifa, mahakama ya ICC haina polisi wake. Inategemea ushirikiano wa Mataifa wanachama, ikiwa ni pamoja na kutekeleza hati zake za kukamatwa au wito.

Wala mahakama haina eneo la kuwahamishia mashahidi ambao wako hatarini. Kwa hivyo, ICC inategemea, kwa kiasi kikubwa, juu ya uungwaji mkono na ushirikiano wa Mataifa.

Vladimir Putin, Rais wa Urusi, akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha sabini cha Baraza Kuu 28 Septemba 2015
UN Photo/Cia Pak
Vladimir Putin, Rais wa Urusi, akihutubia mjadala mkuu wa kikao cha sabini cha Baraza Kuu 28 Septemba 2015

Je, ICJ ina tofauti gani na ICC?

Kuna mkanganyiko wa mara kwa mara kati ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC na Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ.

Njia rahisi zaidi ya kuelezea tofauti ni kwamba kesi za ICJ zinahusisha nchi, na ICC ni mahakama ya jinai, ambayo huleta dhidi ya watu binafsi kwa uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Pia, wakati ICJ ni chombo cha Umoja wa Mataifa, ICC iko huru kisheria na Umoja wa Mataifa ingawa imeidhinishwa na Baraza Kuu.

Ingawa si nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo ni wa ICC, inaweza kutafuta na kufungua kesi na madai ya uhalifu eneo hilo au raia wa nchi wanachama wa ICC au wa nchi ambayo inakubali mamlaka yake.

ICC kesi mbalimbali zimesikilizwa na maamuzi yametolewa kuhusu ukiukaji mbalimbali, kuanzia kutumia ubakaji kama silaha ya vita hadi kuwaandikisha watoto kuwa wapiganaji.

Taarifa zaidi kuhusu ICJ tembelea hapa